Watanzania tumezidi kukosoa

Hapo nimekuelewa labda nikwambie kuna tofauti kati ya kumkosoa na kumkashifu mtu hakuna kiumbebanaeweza kumkosoa mungu isipokuwa kumkashifu
Hata watanzania wengi wanafanya kukashifu mf kusema pombe sio chai wakizani wanakosoa kumbe wanakashifu
 
Tangu mh. JPM kuingia madarakani mengi yameonekana akiwa kama binadamu hakosi madhaifu ila watanzania too much tumezidi kukosoa hatujui hata kusifia nauhakika kuna mtu hapa ukimuuliza jema moja la mh JPM atakwambia hana.
Mwisho wa kuwaza
Kwani kuna kipengele cha katiba kilichovunjwa?
 
Inamaana marais wengine walkuwa hawakosolewi. Hiv kuna rais aliyekosolewa kma kikwete?
 
Kwan mi nimekataa rais kukosolewa tatizo imekuwa too much hata wanaomsifia mh. Nao wanaonekana wamekosea
Ukishavunja katiba hakuna jema litakaloonekana kwakuwa katiba ndiyo sheria mama uliyoapa kuilinda na kuiheshimu sasa kuivunja ni kama kuinajisi. Hakuna kitu kibaya katika utawala kama kubinya haki za raia walizopewana katiba uliyoapa kuilinda. Na katoka uongozi hakuna kitu kibaya kama kutaka wewe ndio mjuaji na suluhisho la kila kitu. Siku ukikwama anguko lako ni kubwa kwakuwa unakuwa huna wa kukutetea na watetezi wengi hufanya kwa unafiki kulinda maslahi yao. Atubu tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…