Siku za karibuni nimekuwa nikisikia maneno ambayo nilidhani ninafahamu vizuri udogo wake, ajabu ninayoipata ni kukuzwa kwa maneno hayo na kusahau yaliyo makubwa zaidi. Sitaegemea mrengo wowote wa kisiasa na nadhani tukijifunza kushughulika na issues badala ya persons au parties, tutakuwa karibu na Tanzania tunayoitaka kuliko hii.
"Vurugu"
Nilijua neno hili kama ugomvi usiokuwa na mpangilio unaohusisha matumizi ya nguvu, vitu vyenye lengo la kuleta maumivu ya mwili au upotevu wa mali. Neno hili sasa linatumiwa kwa yeyote anayejitetea, anayepinga kwa maneno pale anapoambiwa aachane nalo. Yule asiyetaka kuamini neno linalotamkwa na waziri. Tunapaswa kutoka kwenye kutumia neno hilo kwa maana ya kutaka kumzuia mtu kutoa maoni yake, kukataa maoni ya mwingine kwa kushurutishwa nk.
"Uchochezi"
Neno hili sasa linatumika kumwelezea yeyote anayemuelezea mwingine mtazamo tofauti na unaotolewa na serikali. Sasa hivi yeyote anayekataa maelezo au maelekezo ya serikali nae ni mchochezi sawa na anayewashauri au washawishi wengine kupinga serikali au jambo halali. Hii haikubaliki, kuwa tofauti kimawazo na kutaja utofauti wake si uchochezi hata kama anayefanya hivo anaonesha hasira. Ni uchochezi tu kama uongo unatumika kuelezea jambo na katika hili vyama vya siasa vimehusika sana, serikali imechochea kwa kutoa taarifa zisizo na ukweli na zimechochea hasira za wale wanaopingana nazo. Tumeshuhudia uchochezi wa serikali katika maswala kadhaa ya kidini (kuchinja), kisheria (kuzuia mikusanyiko ya watu ambayo ipo kikatiba), kutochukua hatua dhidi ya uhalifu (watekaji wa Kibanda, Ulimboka na mauaji ya Mwangosi). Tufike sehemu tukubaliane kutokubaliana!! Kukataa kuamini jambo fulani na kuonesha huamini, si uchochezi!!! Neno hili limetumiwa na madhalimu wote katika mfumo wa kidikteta ambapo ni watawala tu ndio wanaona wako sahihi na wengine wote sio sahihi na upingaji hadharani wa mawazo ya watawala ni uchochezi wa umma.
"Sera"
Sera ni "policy" ambayo lazima iwe na ideology, strategy na execution plan ili matokeo yake yaonekane mwishoni. Watanzania wa sasa wanajua kiasi kikubwa cha sera za vyama vyetu vya siasa kwa muda mrefu. Lakini utasikia maneno kama haya "CCM au Chadema hawana sera". Na hayo yamesema kila mara wanasiasa wanapolalamikiana. Utasikia "Chadema hawana sera" pale wanapolalamikia Ufisadi, Wizi, dhuluma ya kidemokrasia nk. CCM nao utasikia "ukanda, udini, ukabila nk". Ukiangalia chaka hili linalotumiwa kama "sera" kwa hakika ni uwajibikaji. Tutoke kweny kuangalia maswala ya uwajibikaji kama sera. Tuhoji uwajibikaji bila kutishwa, kwa sababu kimsingi kila chama lazima kiwe na ajenda ya uwajibikaji ili matokeo ya sera zake yaonekane. Tumeshindwa kuhoji uwajibikaji ndio maana tuko hapa tulipo!!!
Tulete mabadiliko haya katika namna tunavofikiria. Wanasiasa wanaoyafahamu haya wanayatumia kama udhaifu wetu na ndio maana wanajipa haki ya kuona tafsiri zao ndio zinazopaswa kutumika.
Tuibadilishe nchi kwa kujibadilisha wenyewe kwanza!!!