Omuchimati
JF-Expert Member
- Aug 23, 2014
- 427
- 202
Namshukuru Mungu kwanza kabisa kwa kunipa uhai na kuniwezesha kupumua hadi leo hii ni wengi nimeshawapoteza ndugu jamaa na marafiki, achilia mbali walioko mahospitalini na jela, hakika ni vyema kumshukuru MUNGU.
Sitaki kwenda nje ya mada hapo juu,watanzani wakati tunamtafuta Rais wa awamu ya tano tulihubiri mabadiliko, nilipita vijiweni huko kinondoni, sinza, Makumbusho kijitonyama, watu wote walikuwa wakihubiri mabadiliko,iliwabidi wanasiasa wacheze kulingana na ala ya wimbo huo nao wakaanza kuhubiri mabadiliko,lakini kumbe tulikuwa hatupo tayari kwa mabadiliko.
Baada ya Mhe John Joseph Pombe Magufuli kuikamata awamu ya tano amesafisha nyumba kwa kuwatimua watumishi walioshindwa kusimamia misingi ya maadili, kwani wengi wao walitumia vyeo vyao kwa manufaa yao wenyewe, achilia mbali watumishi wa umma, wafanyabiashara wabadhirifu na wahujumu wa uchumi, wembe umewagusa wanalia ,wanamlilia Magufuli wanasema anaendesha nchi kwa media, anakurupuka, hana huruma na wafanyabiashara na watumishi wa umma,Je ni mabadiliko gani enyi wana wa Tanzania mliyataka? Mlitaka nchi iendelee kunyonywa na watu wachache? Mlitaka pengo kati ya maskini na matajiri lizidi kuwa kubwa? Nchi isingekalika......amani ingetoweka kwani maskini wangeshindwa kuvumilia,anachokifanya JPM haya ndio mabadiliko ya kweli,mimi namuunga mkono, wewe je?