Watanzania tukiendekeza majadiliano ya kisiasa tutakwama kama Uingereza!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Namsikitikia mkoloni wetu Muingereza baada ya kuona ameingia kwenye tope la kuendekeza midomo isiyochoka ya wanasiasa.
Kwa maoni yangu Uingereza imekwama kimaendeleo kwa sababu moja tu
..yaani kujidai inamsikiliza kila mwanasiasa.
Haipiti miaka miwili au mitatu lazima waitishe kura ambazo zinatumia kodi za wananchi.

Nawasihi sana watanzania waondokane na hulka hii mbaya ambayo inawezekana alituachia.
 
Namsikitikia mkoloni wetu Muingereza baada ya kuona ameingia kwenye tope la kuendekeza midomo isiyochoka ya wanasiasa.
Kwa maoni yangu Uingereza imekwama kimaendeleo kwa sababu moja tu
..yaani kujidai inamsikiliza kila mwanasiasa.
Haipiti miaka miwili au mitatu lazima waitishe kura ambazo zinatumia kodi za wananchi.

Nawasihi sana watanzania waondokane na hulka hii mbaya ambayo inawezekana alituachia.
Demokrasia inalinda amani sana.
Bila demokrasia amani inapatikana kwa ncha ya upanga.

Marekani ingeendekeza Ubabe leo hii kila Jimbo lingekua nchi.

Lakini Marekani bado ni Taifa moja na majimbo yake 52 kwa sababu ya demokrasia.

Kwa sasa hapa Tz wenye siasa Massa 24 ni Serikali na Chama Cha mapinduzi. Wapinzani wamezuiliwa kufanya siasa au hujui hilo.

Wanajua wasipofanya siasa peke yao watapoteza nguvu.
Maandamano ni CCM ,Uchaguzi ni wao wenyewe. Sasa nani unamzungumzia hapo.
Uingereza ni watu wenye uelewa mpana hawakubali kuburuzwa na binadamu mwenzao.
Wenzetu wameshahama kwenye kuwaabudu binadamu wenzao.

Kila mtu anahesabika kama MTU mwingine hivyo ni lazima akosolewe na kupingwa pale panapostahili.

Tanzania Tatizo sio malumbano ya kisiasa Bali kuna shida katika ujenzi wa taasisi imara zinazojiendesha.

Mfano: Kama sio Rais na IGP kuingilia suala la askari waliokua wanatorosha madini kwa rushwa nani angejua! Sasa jiulize kama watu wanafikia mahali wanapeana mapesa mengi kiasi hicho wakati walikua wanatakiwa kufuata taratibu na kulipa lodi ambayo huenda ingekua ni ndugo kuliko hiyo bil.1 iliyokua iishie mifukoni mwa watu wachache. Bil. Inajenga madarasa kumi ya shule.

Sasa jiulize mtu mwenye mshahara usiofika mil. 1.5 anadai rushwa ya bil. 1 na pesa inatika kama vipe ni business as usual nini tatizo? Bila shaka Tatizo ni kukosekana kwa taasisi imara ya kuzuia na kupambana na Rushwa lakini pia Tume ya maadili imepewa wigo mdogo.

Wala rushwa kama hao wapo idara nyingi. Sasa watu wanacheza madili makubwa kabisa ya matri bila Hofu mana hakuna wa kuwahoji wala kuwachunguza.

Mtu mshahara laki NNE halafu kwa miaka miwil anajenga nyumba yenye thamani ya mil. 200 na gari la kifagari na mke wake watoto wanasoma shule za Private n.k. Hapo panahitaji mpaka Mh. Mkuu wa nchi apewe taarifa kweli ?
Tatizo ni taasisi imara zenye uwezo wa kuchunguza watumishi wa umma ili kujenga maadili mema na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma.

Hayo hapo kila sekta,TRA wapo, Sumatra wapo, uhamiaji wapo ,maliasili wapo, Takukuru wapo ,Mahakamani wapo,toss wapo , kwenye ulinzi wapo, Bandarini wapo, mifuko ya jamii wapo, Huko halimashauri wapo. Wizara ya ardhi wapo n.k.
Wangekua wanaulizwa ndugu hebu tuambie mwenzetu umepata wapi pesa za kujitajirisha kwa haraka hivi ? Nadhani pangekua na hofu kidogo!

Idara zinazohusika zijengwe na kusukwa vizuri sana kitaasisi ili zimsaidie Rais mana vita ya rushwa na uhujumu uchumi ni kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uingereza haijakwama na wala haitakaa ikwame.Akili yako fupi haiwezi kufanya tathmini kwa siasa za taifa makini kama lile lililowahi kukutawala wewe na karibu mbili ya tatu ya dunia.Wanasiasa na raia wa Uingereza wamekuwa wakifanya majadiliano na midahalo kwa karne nyingi na kwa mambo mengi,wameweza kutoka katika tawala ya mfumo wa kifalme hadi demokrasia bora zaidi duniani na wakabaki imara, Brexit ni kama kunywa maji kwao.
Je uingereza haijakwama?
Je wanasiasa wa Uingereza hawalumbani?
 
Siku ukiamua kuwa mtanzania utauona mwanga, lakini ukiendelea kuwa raia wa kigeni utawaona watanzania wajinga sana na wewe na raia wenzio wa kigeni ndio mna akili...
 
lazima waitishe kura ambazo zinatumia kodi za wananchi.
Wanafiki wakubwa mnajifanya kuwa na huruma na matumizi mabaya ya kodi za wananchi wa uwingereza badala ya kuhurumia kodi za watanzania ambazo mnazitumia kununua wapinzani tumbo na kurudia uchaguzi kwa kutumia kodi hizo hizo za wananchi.
 
Back
Top Bottom