Watanzania tukiendekeza majadiliano ya kisiasa tutakwama kama Uingereza!

Demokrasia inalinda amani sana.
Bila demokrasia amani inapatikana kwa ncha ya upanga.

Marekani ingeendekeza Ubabe leo hii kila Jimbo lingekua nchi.

Lakini Marekani bado ni Taifa moja na majimbo yake 52 kwa sababu ya demokrasia.

Kwa sasa hapa Tz wenye siasa Massa 24 ni Serikali na Chama Cha mapinduzi. Wapinzani wamezuiliwa kufanya siasa au hujui hilo.

Wanajua wasipofanya siasa peke yao watapoteza nguvu.
Maandamano ni CCM ,Uchaguzi ni wao wenyewe. Sasa nani unamzungumzia hapo.
Uingereza ni watu wenye uelewa mpana hawakubali kuburuzwa na binadamu mwenzao.
Wenzetu wameshahama kwenye kuwaabudu binadamu wenzao.

Kila mtu anahesabika kama MTU mwingine hivyo ni lazima akosolewe na kupingwa pale panapostahili.

Tanzania Tatizo sio malumbano ya kisiasa Bali kuna shida katika ujenzi wa taasisi imara zinazojiendesha.

Mfano: Kama sio Rais na IGP kuingilia suala la askari waliokua wanatorosha madini kwa rushwa nani angejua! Sasa jiulize kama watu wanafikia mahali wanapeana mapesa mengi kiasi hicho wakati walikua wanatakiwa kufuata taratibu na kulipa lodi ambayo huenda ingekua ni ndugo kuliko hiyo bil.1 iliyokua iishie mifukoni mwa watu wachache. Bil. Inajenga madarasa kumi ya shule.

Sasa jiulize mtu mwenye mshahara usiofika mil. 1.5 anadai rushwa ya bil. 1 na pesa inatika kama vipe ni business as usual nini tatizo? Bila shaka Tatizo ni kukosekana kwa taasisi imara ya kuzuia na kupambana na Rushwa lakini pia Tume ya maadili imepewa wigo mdogo.

Wala rushwa kama hao wapo idara nyingi. Sasa watu wanacheza madili makubwa kabisa ya matri bila Hofu mana hakuna wa kuwahoji wala kuwachunguza.

Mtu mshahara laki NNE halafu kwa miaka miwil anajenga nyumba yenye thamani ya mil. 200 na gari la kifagari na mke wake watoto wanasoma shule za Private n.k. Hapo panahitaji mpaka Mh. Mkuu wa nchi apewe taarifa kweli ?
Tatizo ni taasisi imara zenye uwezo wa kuchunguza watumishi wa umma ili kujenga maadili mema na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma.

Hayo hapo kila sekta,TRA wapo, Sumatra wapo, uhamiaji wapo ,maliasili wapo, Takukuru wapo ,Mahakamani wapo,toss wapo , kwenye ulinzi wapo, Bandarini wapo, mifuko ya jamii wapo, Huko halimashauri wapo. Wizara ya ardhi wapo n.k.
Wangekua wanaulizwa ndugu hebu tuambie mwenzetu umepata wapi pesa za kujitajirisha kwa haraka hivi ? Nadhani pangekua na hofu kidogo!

Idara zinazohusika zijengwe na kusukwa vizuri sana kitaasisi ili zimsaidie Rais mana vita ya rushwa na uhujumu uchumi ni kubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujui kitu,huko US kuna majimbo hadi Leo wanatamani kujitenga Ila katiba yao imeweka wazi kuwa yeyote atakayethubutu kufanya hivyo hukumu yake ni kifo kwa kesi ya uhaini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namsikitikia mkoloni wetu Muingereza baada ya kuona ameingia kwenye tope la kuendekeza midomo isiyochoka ya wanasiasa.
Kwa maoni yangu Uingereza imekwama kimaendeleo kwa sababu moja tu
..yaani kujidai inamsikiliza kila mwanasiasa.
Haipiti miaka miwili au mitatu lazima waitishe kura ambazo zinatumia kodi za wananchi.

Nawasihi sana watanzania waondokane na hulka hii mbaya ambayo inawezekana alituachia.
Ingependeza kama wangekuwa na serikali ya kidikteta kama China.
 
Hujui kitu,huko US kuna majimbo hadi Leo wanatamani kujitenga Ila katiba yao imeweka wazi kuwa yeyote atakayethubutu kufanya hivyo hukumu yake ni kifo kwa kesi ya uhaini

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unajua lakini huna akili ya kutafakari mambo kwa usahihi.
Unashikiwa akili nawanasiasa kwa kutafuta maslahi na ishabiki usio na mbele wala nyuma ndio maana Waafrika hatuendelei mana hatujui mema na mabaya .

Marekani ni mchanganyiko wa Watu asili tofauti tofauti.
Udikteta hauwezi kamwe kuitawala Marekani. Sheria ya uhaini hata urusi ilikuwapo lakini ilisambaratika mana hawana asili moja wote.
Hata hapa Tanzania udikteta ulishindikana tangu Mkoloni.
Mkiloni alishindwa kuitawala Tanzania bila kuwatumia machief wenyeji.

Haiwezekani kabila moja na dini moja na familia moja kutawala makabila 125 bila kushirikisha makabila mengine na dini nyingine.

Makabila au moja ndilo linaloweza kutawaliwa kidikteta mana wanakua kama Familia moja au Kabila moja lenye nguvu liwaue wale wenye asili ya utawala wa Kabila la pili ili kuwatia hofu waliobaki na kukubali kuwa chini ya udikteta. Kama ilivyotokea Rwanda.

Tumia akili yako na ujuaji wako sawa sawa.

Tofautisha kutaka kujitenga na kuanzisha vita ya kutafuta Uhuru toka kwenye mikono ya Kikteta.
Mabuto aliendesha nchi kidikteta matokeo yake mpaka Leo kuna vita Kongo.

Watu wanapozidi kupata elimu na kuwa na maisha ya kisasa wanazidi kujua haki zao kwa hiyo usitegemee kuwa udikteta una nafasi huko Mbele dunia inakoelekea.

Dunia imetokea kwenye zama za Giza na ujinga ndipo wajanja wachache wakishirikiana na wale wenye maguvu walipowatawala watu Kidikteta. Muda unavyozidi kusogea madikteta wanabaki wachache na muda sio mrefu watabaki historia.
Kila mtu anatamani madaraka na maisha mazuri sio familia moja tu na marafiki zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namsikitikia mkoloni wetu Muingereza baada ya kuona ameingia kwenye tope la kuendekeza midomo isiyochoka ya wanasiasa.
Kwa maoni yangu Uingereza imekwama kimaendeleo kwa sababu moja tu
..yaani kujidai inamsikiliza kila mwanasiasa.
Haipiti miaka miwili au mitatu lazima waitishe kura ambazo zinatumia kodi za wananchi.

Nawasihi sana watanzania waondokane na hulka hii mbaya ambayo inawezekana alituachia.
Hebu tuambie, wewe unataka waendeshe vipi nchi yao? Demokrasia imewawezesha wamefika hapo walipo. Mambo mengi unayosoma kwenye sayansi waligundua wao. Sisi kwa ujinga, tunajidai wajuaji, tunaenda kujifunza utawala kwa wanyarwanda wanaotambulika zaidi kwa genocide. Hata aibu hatuoni, tunafikiri wahutu na watusi wanajua utawala zaidi ya waingereza?

Shame
 
Hebu tuambie, wewe unataka waendeshe vipi nchi yao? Demokrasia imewawezesha wamefika hapo walipo. Mambo mengi unayosoma kwenye sayansi waligundua wao. Sisi tunajidai wajuaji sana kwa kuiga kwa wanyarwanda aina za utawala za wanaotambulika zaidi kwa genocide.
Wasiendekeze siasa warudi kwenye sayansi...
 
Uingereza haijakwama na wala haitakaa ikwame.Akili yako fupi haiwezi kufanya tathmini kwa siasa za taifa makini kama lile lililowahi kukutawala wewe na karibu mbili ya tatu ya dunia.Wanasiasa na raia wa Uingereza wamekuwa wakifanya majadiliano na midahalo kwa karne nyingi na kwa mambo mengi,wameweza kutoka katika tawala ya mfumo wa kifalme hadi demokrasia bora zaidi duniani na wakabaki imara, Brexit ni kama kunywa maji kwao.
Mtaelewa tu
 
Namsikitikia mkoloni wetu Muingereza baada ya kuona ameingia kwenye tope la kuendekeza midomo isiyochoka ya wanasiasa.
Kwa maoni yangu Uingereza imekwama kimaendeleo kwa sababu moja tu
..yaani kujidai inamsikiliza kila mwanasiasa.
Haipiti miaka miwili au mitatu lazima waitishe kura ambazo zinatumia kodi za wananchi.

Nawasihi sana watanzania waondokane na hulka hii mbaya ambayo inawezekana alituachia.
Uingereza bado ni taifa lenye uchumi mkubwa duniani kuliko wa bara lote Africa combined together. Lakini siioni future ya uingereza . Democrasia imezidi mno . Kiongozi hakai Sana madarakani anakwamishwa kwahiyo anamaliza mda kabla hajatekeleza ahadi zake
 
Wanatania maisha ya watu
 
Kama Uingereza inakusumbua na unaota nchi yako kuipita siku moja kajifunze kwa Italia, Israel na Japan ambazo mawaziri wake wakuu kudumu zaidi ya miaka mitatu tu mfufulizo ni nadra kama kuona mvua jangwani.Mataifa yaliyostaaribika na kujielewa serikali zao ni 'taasisi imara' sio 'one man show'

Back
Top Bottom