Watanzania tujitoe kifungoni

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
10,344
14,120
nionavyo Mimi watanzania tupo vifungoni kama tujuavyo kwa wafungwa mwenye mamlaka ya kumuendesha mfungwa hakuna zaidi ya bwanajela. hivyo hivyo sisi tupo kama wafungwa ambapo viongozi na matajiri ndio mabwana jela wetu.

Si kitu kigeni Leo tajiri kuwahamisha watu pasipo kufata Sheria..si kitu kigeni viongozi wenye madaraka makubwa Leo kujimilikisha ardh zaidi ya heka 100 Mungu alitupa watanzania hadhina kubwa kuliko nchi yoyote duniani...tuna migodi Mikubwa mikubwa, mbuga zaidi ya tano kubwa, milima mikubwa maziwa kila kona, bandari, gesi nk.

Hivi vyote tusinge vitumia mpaka tupate elimu hayo yangekuja kunufaisha wajukuu zetu..lakini kutokana na ufinyu wa maarifa wa viongozi wetu na kujifanya wao NI wagunduzi wanaamua kugawa rasilimari zetu huku na huko wageni wananufaika...Ila tukae tufikirie miaka 50 wajukuu zetu watarisi nini? Mimi nawewe Leo tunawachekea viongozi wabovu ambao wanatusababishia laana kwa makusudi kabisa.

Ingekuwa ni mamlaka yangu ningesimamisha uchimbaji wa madini na uvunaji wa gesi kwasababu hatuna ujuzi wa kutosha juu ya matumizi ya vitu hivyo...
 
Mkuu, umeeleza machungu yako hujasema nini tufanye ili kutoka gerezani. Umesema 'Ingelikuwa wewe ni mtawala' sasa sisi wengine je...??
 
Mkuu, umeeleza machungu yako hujasema nini tufanye ili kutoka gerezani. Umesema 'Ingelikuwa wewe ni mtawala' sasa sisi wengine je...??
kwa ujumra tuiombe serikali isitishe uchimbaji wa madini na uvunaji wa gesi hadi pale tutapopata wataalam wa kutosha
 
upo sahihi tupo jela zaidi watawala wanaona sehemu ya kupata kodi ni kutoka katika magari aina zote kodi yake ni kubwa kuriko hata kiwango cha kodi katika madini au gesi kutwa kujisifia kukamata mali za watanzania ili zipigwe mnada huku kaburu akibeba madini kwa kodi ambayo ni chenji tuu..
 
Back
Top Bottom