Watanzania tujifunze kitu kutoka Kenya

Watanzania tujifunze kitu kutoka Kenya

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
123,293
Reaction score
98,356
Ndugu zangu wana jf nimeweka hii picha kama kichocheo cha kujenga upendo na mshikamano wa taifa letu,nini maoni yako?hiyo picha ni ya leo hii jijini Nairobi
FB_IMG_1521992729557.jpg
 
Huku kwetu tanzania kuna mtu mwenye dharau na inda sana hawezi fanya anayofanya Uhuru Kenyatta.
Yote mnayasababisha ninyi wananchi kwa kumshobokea huyo mtu mkataeni
 
Tatizo letu in mambo matatu(1) Ccm- kwa baadhi ya watu ccm ni muhimu kuliko Tanzania (2) exposure (3) Elimu
Hayo mengine yote ni porojo tu, tatizo ni ELIMU pekee, PhD au U profesa sio kipimo cha ELIMU. PhD na U profesa wao ni FEKI FEKI. Mwangalie Mwakyembe, Kahabudi, Pogba mwenyewe, Migulu, orodha ni ndeefu
 
Bi. mchoma maandazi.
 
Tatizo letu in mambo matatu(1) Ccm- kwa baadhi ya watu ccm ni muhimu kuliko Tanzania (2) exposure (3) Elimu
eee bana eee. Hatimae mkuu umetaja sababu au tatizo kuu la watanzania wengi. Hiyo namba mbili umepatia sana. Yeap exposure ndio shida kubwa kwenye vichwa vya sisi watanzania wengi. Na ii imetuchelewesha sana hata kustaarabika katika baadhi ya maeneo. Karne hii bado kuna jamii zinazohamasishwa umuhimu kuchimba na kutumia choo. MMMMh
 
Degree, PhD is only a receipt that you paid that money to study. The real school is in society. When you find a job and prove really makes things different.
 
shida magufuli hata akikutana na wanasiasa wa upinzani katika mazingira ambayo sio ya kupiga siasa, yeye hupiga vijembe vya kisiasa na hatimaye kuacha maudhi na maswali mengi.

rejea tukio la ile siku alipotembelewa ikulu na lowassa.
 
Sio Magufuri tu yaani mfumo wa maisha yetu umetufanya tumeshindwa kubadilika kwenda na mazingira ya sasa ya kisiasa wakati kila kitu kipo wazi tangu mwaka 1992 mara baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi...kuna watu wanashindwa kutofautisha Serikali na chama kilichoshika dola na ndio maana hata kama kuna mbunge au kiongozi ametokea chama cha upinzani ambae amechaguliwa na wananchi akionekana yupo karibu na serikali (watu wa wanashangaa)

Nchi yetu hii tukiondoa haya maneno kwenye shughuli rasmi za serikali mfano "serikali yangu ya CCM" na kuweka serikali ya Jamhuri ya Tanzania (ila kwenye majukwaa ya kisiasa kama mikutano ya chama hata ukisema serikali ya CCM hapo its okay kwa kuwa unataka kuonyesha mafanikio)

Au unamtambulisha Mbunge ambae amechaguliwa na wananchi kwa kusema Kadoda11 ..Mbunge wa CHADEMA au Jodoki Kalimilo ...Mbunge wa CCM. Badala yake tukawatambulisha kwa majimbo yao mfano Kadoda11 Mbunge wa Njombe au Jodoki Kalimilo Mbunge wa Kilosa (hii imekaa Kitaifa zaidi kwa kuwa hawa wabunge ni wanachama wa vyama hivyo ila wamechaguliwa na wananchi kuwawakilisha na mtu akitaka kujua wanatoka vyama gani ni yeye mwenyewe sasa anakuwa ana-interest zake)

Lakini sie uchaguzi umeisha walioshinda wameshinda lakini wanapokuwa kwenye majukumu yao ya kiuongozi kama wawakilishi wa wananchi, watu bado wanaleta issue za siasa
 
eee bana eee. Hatimae mkuu umetaja sababu au tatizo kuu la watanzania wengi. Hiyo namba mbili umepatia sana. Yeap exposure ndio shida kubwa kwenye vichwa vya sisi watanzania wengi. Na ii imetuchelewesha sana hata kustaarabika katika baadhi ya maeneo. Karne hii bado kuna jamii zinazohamasishwa umuhimu kuchimba na kutumia choo. MMMMh
Harafu eti kuna watu wanategemea Tanzania ya viwanda,how wakati hata Vitu basic kama choo au kunawa mikono tukitoka chooni bado tunasubiria mzungu aje na project kutufundisha umuhimu wake,shame on us
 
Back
Top Bottom