Watanzania tuhamie wapi?

Watanzania tuhamie wapi?

Isango

R I P
Joined
Jul 23, 2008
Posts
295
Reaction score
450
Operesheni ya kutokomeza majangili inavyotuangamiza, inavyotutesa. Hawa ni wakaazi wa Wilaya ya Singida waliochomewa nyumba kwa utekelezaji wa operesheni hiyo maeneo ya Mgori. Kwanini watu wanaitwa wavamizi wa maeneo waliyokaa tangu utoto wao miaka mingi? Tumekosea wapi kwanini serikali inatutesa? Hivi tukiangalia kati ya hawa kuna mtu hatari kwa wanyama hata digidigi? Kwanini wanaonufaika na Tembo ndio wanaoandaa mateso kwa wasio na mateso?.... Watetezi wa haki za binadamu, watetezi wa akina mama, watetezi wa watoto fikeni saidieni suala hili. Serikali ndio imewatendea hivi wakimbilie wapi?. Tuhamie wapi?
 

Attachments

  • bibi.JPG
    bibi.JPG
    352.1 KB · Views: 97
  • wakiwa korongoni.JPG
    wakiwa korongoni.JPG
    2.8 MB · Views: 91
Akina mama tumeikosea nini serikali ya CCM? kwanini tunateswa hivi? kutufanyia sisi hivi ndio kunusuru tembo? Tembo mbona hawapo kwenye nyumba zetu, kwanini nyumba zimechomwa mahali tunapoishi siku zote........ machozi.
 
Si wa hurumii hata kidogo. Hao ndio kila mara wakipewa khanga wanaipigia kura CCM. Ngoja waonje utamu wake sasa!!!!

Tiba
 
DC wa Singida ndiye aliyeruhusu ukatili huu dhidi ya akina mama. Mkuu wa Wilaya mwenyewe mwanamke, wanawake tunaweza! amemvimbia naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kuteketeza nyumba za watu.
 
Hapo hakuna ukatili. wanavuna walichopanda... Hii ni faida ya kuing'ang'ania CCM...
 
Dc wa Singida usichome nyumba tu!.... Timiza maagizo ya Pinda.... Pigaaaa!... Usiangalie sura wala jinsia piga tuu!... Maana serikali imechoka!
 
Serikali ya CCM imefilisika kimawazo kabisa, na imekuwa kama kipofu anaetembea peke yake bila msaidizi...kwanini uwahamishe wananchi kwa kuwadhalilisha kiasi hicho? hawa ni wakulima maisha yao yote yanategemea kilimo, sasa msimu wa kilimo umeanza halafu serikali inawabomolea nyumba kwa kuzichoma moto, hawa wananchi wataishi vipi mwaka mzima huu?
Wananchi wa Singida na Tanzania tuamke sasa, hii sio serikali yetu bali ukoloni....tufanye mabadiliko kujikomboa wenyewe...
SHEM ON YOU CCM AND UR GOVNT
 
Hiyo ndiyo ari mya, nguvu mpya na kasi mpya! Chagua CCM tena 2015.
 
Back
Top Bottom