Watanzania tufunge mkanda, kipindi kigumu zaidi kinakuja

Tujue hata historia kidogo.

Kuna mawaziri wakuu na marais ambao walikua wanaua wananchi wao actively. Wanabana demokrasia wanakuwinda wewe na ndugu zako na ukoo wako wote mnapotezwa.

Kisha rais wa marekani anamualika huyo kiongozi wanakunywa shampein kiongozi anarudi nchini kwake kuendeleza mabalaa.

Recent example ni aliyewahi kua PM wa Thailand.

You see wenzetu wanaongozwa na kanuni ya 'Mutual benefit' ambayo hupelekea wasiwe na rafiki au adui wa kudumu. Kama ccm itaoffer benefit kwa hizo nchi wahisani hata kama Tz tutakua tunapokea bakora mbili mbili asubuhi na jioni hakuna atakayejali.
 
Nafikiri watu waliposema CHADEMA imekufa mlidhania wanatania? Sasa matokeo yameanza kutoka mnaanza kuliombea mabaya taifa letu.
 
#Tufunge Mikanda: Hizi ni akili finye, kwahiyo upinzani ukishinda ndio misaada inatolewa na wahisani.

Wanaotoa misaada pia hufunga mikanda kuzalisha zaidi ili ziada wasaidie wenye uhitaji.
Wapinzani walifanya kosa kubwa sana kufanya kampeni za kumshambulia Rais aliye madarakani wakati wakijuwa walikuwa wakimwonea kwa nia ovu lakini Watanzania ndio wanaochagua.
Hakuna sehemu yoyote mtu alitishwa kuchagua 'the incumbent president' na kusuasua kuonesha sauti zao kuchagua Rais mbadala kutoka upande kinzani.
Hakuna wa kumlaumu hapa kwa sababu waajiri wakubwa ni wananchi ambao ndio wanadhihirisha matokeo ya sasa.
Kila upande unatakiwa kuchunga ndimi kumsemea uongo mwingine ilihali ukijua unamkosea hukumu yake ndio hii tunayoina kutoka kwenye sanduku la kura.
Tume ya uchaguzi imesimamia vizuri sana kuliko wakati wowote tangu 1995 ambapo kila hatua wapiga kura wamepewa nafasi sawa, mawakala wakiwepo kushuhudia na kukiri kiilichotokea ni uamuzi halali wa wananchi wenyewe.
 
Nchi yetu ni moja ya nchi inayopkea misaada na mikopo mingi kutoka nchi wahisani na mashirika ya fedha ya kimataifa kuendeshea miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo hapa nchini.

Fedha hizi,hasa misaada,zinatusaidia kupunguza nakisi ya Bajeti lakini pia zinatupa uwezo wa kulipa deni la Taifa kwa kufidia hela tunazotumia kuhudumia hilo deni ambalo teyari ni kubwa mno.

Miradi mingi kama ule wa Ubungo interchange na miradi mingine mingi inagharamia na fedha za mikopo kutoka Benki ya Dunia na shirika la fedha la kimataifa(IMF).

Pia,huduma nyingi za kijamii kama afya,maji na elimu zinaendeshwa kwa misaada ya nchi wahisani kupitia mashirika yao ya misaada au kutoka katika serikali hizo moja kwa moja.

Na wakati huo huo tukumbuke sehemu kubwa ya makusanyo yetu yanatumika kulipa mishahara ya wafanyakazi na kuhudumia deni la Taifa.

Sasa,kwa jinsi tulivyoendesha huu uchaguzi kwa uporaji wa wazi wa matakwa ya wananchi na kwa kupuuza wazi wazi ushauri na wito wa nchi wahisani wa kutaka tuwe na uchaguzi ulio huru na wa haki,kitachofuata ni nchi hizi na mashirika yao ya fedha kukata misaada na mikopo huku tukiwa hatujajiandaa kukabiliana na hali hiyo na mwananchi wa kawaida ndio atakwenda kubeba mzigo huu wa maumivu huku CCM na serikali yake wakibeba gharama ya anguko la kisiasa wananchi watapoanza kuumia.

Hivyo,watanzania tujifunge mkanda angali mapema kukabiliana na magumu yatayotokana na huu uchaguzi kwani kidogo tunachokusanya ndio kitatumika kuendeshea serikali, kulipa madeni, kugharamia huduma za Jamii na miradi mbalimbali.

Halikadhali, sitashangaa kuona baadhi ya miradi ikikwama kuendelea huko mbeleni na pia tusiwe kabisa na miradi mipya ndani ya hii miaka mitano ijayo au tukawa nayo kwa kusuasua.

Nje ya mada ila mule mule:Mtarajie na Bunge live kurudi.

Time will tell.
[/QUOTE

Miaka mitano ijayo magufuli anaenda kuifanya Tanzania iwe na maendeleo kuzidi hata nchi za Ulaya magharibi
 
Nchi yetu ni moja ya nchi inayopkea misaada na mikopo mingi kutoka nchi wahisani na mashirika ya fedha ya kimataifa kuendeshea miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo hapa nchini.

Fedha hizi,hasa misaada,zinatusaidia kupunguza nakisi ya Bajeti lakini pia zinatupa uwezo wa kulipa deni la Taifa kwa kufidia hela tunazotumia kuhudumia hilo deni ambalo teyari ni kubwa mno.

Miradi mingi kama ule wa Ubungo interchange na miradi mingine mingi inagharamiwa na fedha za mikopo kutoka Benki ya Dunia na shirika la fedha la kimataifa(IMF).

Pia,huduma nyingi za kijamii kama afya,maji na elimu zinaendeshwa kwa misaada ya nchi wahisani kupitia mashirika yao ya misaada au kutoka katika serikali hizo moja kwa moja.

Na wakati huo huo tukumbuke sehemu kubwa ya makusanyo yetu yanatumika kulipa mishahara ya wafanyakazi na kuhudumia deni la Taifa.

Sasa,kwa jinsi tulivyoendesha huu uchaguzi kwa uporaji wa wazi wa matakwa ya wananchi na kwa kupuuza wazi wazi ushauri na wito wa nchi wahisani wa kutaka tuwe na uchaguzi ulio huru na wa haki,kitachofuata ni nchi hizi na mashirika yao ya fedha kukata misaada na mikopo huku tukiwa hatujajiandaa kukabiliana na hali hiyo na mwananchi wa kawaida ndio atakwenda kubeba mzigo huu wa maumivu huku CCM na serikali yake wakibeba gharama ya anguko la kisiasa wananchi watapoanza kuumia.

Hivyo,watanzania tujifunge mkanda angali mapema kukabiliana na magumu yatayotokana na huu uchaguzi kwani kidogo tunachokusanya ndio kitatumika kuendeshea serikali, kulipa madeni, kugharamia huduma za Jamii na miradi mbalimbali.

Halikadhali, sitashangaa kuona baadhi ya miradi ikikwama kuendelea huko mbeleni na pia tusiwe kabisa na miradi mipya ndani ya hii miaka mitano ijayo au tukawa nayo kwa kusuasua.

Nje ya mada ila mule mule:Mtarajie na Bunge live kurudi.

Time will tell.
2015 watanzania wengi sana waliondoka nchini, nadhani mwaka huu mpaka 2021 wengi zaidi wataikimbia nchi
 
Bunge litarudishwa kuwa "Live", kwasababu ya kuongozwa na Utawala wa kimasikini kifikra.

Nchi itaawaliwa kwa mawazo ya mtu mmoja, anaejiona malaika hakosei, anaejiona ana akili kuliko hata Ma Proffesor waliomfundisha.

Hatoboi mpaka 2025. Watamng'oa.
We are in trouble
 
Kipindi cha mateso kwa watanzania chaja. Mwenye kupuuza na apuuze.

Wafanyakazi hawataongezewa mishahara, wakiongezwa, wataongezewa karatasi lakini siyo fedha.

Shilingi itadidimia kwa kasi, na fedha ya kigeni haitapatikana mikononi mwa mwananchi. Na kutokana na upungufu wake, kuipata itakuwa kwa kuomba, na ukikutwa nayo, itakuwa ni hatia.

Elimu itadorora kwa kukosa funding. Installment ya pili ya fedha ya elimu toka WB haitapatikana kama ilivyotarajiwa.

Haitazidi miaka miwili, inflation itakua na kufikia double digits, na kuzifanya bidhaa zinazotoka nje ya nchi kutonunulika.

Watanzania wengi wenye uwezo kifedha na hata baadhi ya wasio na uwezo mkubwa, watatapakaa mataifa jirani kutafuta maisha.

Hakutakuwa na uwekezaji kutoka nje, na wawekezaji wa nje na ndani waliopo, watazidi kuondoka, na kusababisha tatizo kubwa la ajira. Kutokana na tatizo kubwa la ajira, hata watakaokuwa kwenye ajira, maslahi yao yatakuwa duni kupindukia.

Wafanyakazi pekee watakaoonekana ni muhimu kuliko wote ni Polisi, wanajeshi, magereza na wasiojulikana. Hawa watatumika vilivyo katika kuzima sauti yoyote itakayotaka isikike dhidi ya mtawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom