Ndugu zangu amani amani iwe nanyi, nimefatilia kauli za viongoz wetu wa kitaifa wa serekali ya kwamba tufunge mikanda tupo vitani. vita inayoongelewa hapa ni vita vya uchumi na mafisadi. Nimekata tamaa maana si kweli kwamba viongozi wetu wana hali ngumu kimaisha kama tulionayo wakulima, wafanyakazi na wafanyabiasha. kwani viongozi hawa wengi wao mishahara inaanzia milion7 kwenda juu, huyu mtu ana shida gani mpaka atoe povu na kumwonea huruma masikini wa nchi hii. Pili hali mbaya ya uchumi na maisha duni inayotukabili leo watanzania tumeletewa na wakoloni weusi (CCM) ambao wamejitukuza na kujifanya miungu watu. Mafisadi wanaopigiwa kelele leo wamelelewa na kufundishwa wizi na ccm na bado tunaaminishwa kwamba kuna mwizi mtakatifu ambae hapaswi kusemwa wala kushitakiwa, na kuna mwizi shetani ambae anasemwa na kushtakiwa hapa ndo tulipofika watanzania. Ingekuwa vema viongozi wetu waache unafiki na kuwa wakweli kwamba umasikini wetu na udumavu wa akili umesababishwa na ccm kwa kushirikiana na wezi wa kimataifa pia kama kweli mtukufu ana nia njema na taifa hili asiwakingie kifua wezi wakuu waliopo ndani ya chama chake akumbuke hii nchi ni ye2 zote na si mali ya cmm. Hali ya maisha imekua ngumu mno mnadhihaki watu warudi vijijini wanaenda kuishi vipi, watapata wapi mashamba, mbegu na pembejeo. watanzania nawakumbusha2 tabu zetu, umasikini wetu na ulofa tulio nao umesababishwa na wanaccm, neno langu liwabariki. amin.