watanzania tufanye hivi

Ibrahim K. Chiki

JF-Expert Member
Apr 5, 2011
594
163
Wadau, kiukweli inauma kuona tunaigawa tz yetu kichama. mimi ni mpinzani na nawakulabali sana chadema kwa sababu zangu binafsi na si tu kishabiki. kwa mfano, ilani na mikakati ya chadema inalenga kumkomboa mwananchi wa kawaida, ukilinganisha na ilani na mikakati ya ccm, inauma kuona wabunge wetu bungeni wakiendekeza uchama ndani ya bunge? wakipigia kura na kupitisha hoja ambazo kiukweli hazimlengi mtanzania wa kawaida..? hii inadhihirisha kwamba hata tukisema tupambambane kuleta mabadiliko kwa kuchagua rais kutoka upinzani itakua bado ni bure, la msingi hapa ni kupambambana na kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni hata kufikia 70%, hapo tutaweza. Kaaa chini tafakari kwa umakini. nawakilisha.
 
maneno yako yana ukweli ndani yake..... kama chama tawala hakitaondoka madarakani.. wapinzani wajitahidi kuwa na viti vingi bungeni .. mambo yatakuja kukaa sawa mungu akipenda
 
wakati wa maneno umekwisha kilichobakia sasa ni vitendo tafuta namna ya kuisaidia chadema kuanzia leo hii usisubiri wakati
wa uchaguzi it will be too late. chadema ifungue mfuko maalum wa saidia chadema ishinde 2015 ili sisi maskini tuanze mapema
kuchanga shs.500 zetu kila tunapopata ili ikifika 2015 tuwe tumefikia kiasi kikubwa cha kuweza kutufikisha mbali nafikiri chadema
watakuwa wameliskia hili na watalifanyia kazi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom