Mkono Mkavu
Member
- Dec 22, 2016
- 70
- 70
Wakati wa awamu ya kwanza baada ya uhuru,dunia ilikuwa imegawanyika katika makundi mawili yaliyozaliwa na kilichoitwa vita baridi,kulikuwa na kundi lililokuwa linafuata falsafa za mataifa yaliyokuwa yakiamini katika ujamaa yakiongozwa na USSR na yalikuwepo yaliyoegemea kwenye upande wa walioamini katika ubepari!.
Mataifa yaliyoamini katika mlengo wa kushoto yalikuwa katika vita baridi na yale ya mlengo wa kati,hata watu waliotoka huku Afrika waliokwenda kusoma kwenye nchi za mlengo wa kushoto hawakuweza kukaa meza moja na wale waliokwenda kusoma kwenye nchi za mlengo wa kulia!.
Misimamo hii ndiyo iliyowagombanisha Mwalimu Nyerere na akina Kambona,Masha na Kasangatumbo!Upinzani wao kimtazamo ulikuwa mkali kweli kweli!.
Mwalimu alijitahidi sana kuuzima ubepari nchini,ubepari ulifundishwa kuwa ni unyama kuanzia shule za msingi mpaka chuo kikuu,kampeni kali za mwalimu zilizaa wafuasi wengi wa ujamaa akina Profesa Shivji,Marehemu Profesa Chachage Seth Chachage, Marehemu Profesa Haroub Othman ,hawa akina Chachage ndiyo waliowazaa kiitikadi akina Zitto Kabwe pale chuo kikuu cha Dsm!
Wakati huo wa vita baridi,suala la mahusiano ya kimataifa lilijengwa ama kutengenezwa na milengo ya kiitikadi(Political diplomacy),yapo mataifa machanga yaliamua kutokuwa na upande ikiwemo Tanzania,ambao tulijitambulisha kuwa nchi isiyo na upande!.
Baada ya kuyumba ya ujamaa na kufa kwa USSR,wabobezi wa siasa za kimataifa na misimamo ya kiitikadi walizalisha mfumo mpya waliouta mlengo wa kati,hawa walidai wao wanachukua mazuri na ujamaa na ubepari na kuyatekeleza!.
Kufa kwa vita baridi kulizaa mfumo mpya wa mahusiano ya kimataifa,mataifa haya yakaanza kujenga mahusiano kwa kutazama zaidi fursa za kiuchumi(Economic Diplomacy).
Leo mchina akina kwako,haji kwa sababu eti katiba inasema sisi ni wajamaa,anakuja huku kwa sababu anajua tuna ardhi bikra karibu asilimia 40,tuna gesi,misitu,dhahabu,samaki,tanzanite,makaa ya mawe,urenium,mafuta na kadhalika!.
Sawa na anavyokuja Mmarekani,Mkorea,Mfaransa,anakuja hapa kwa sababu anajua kuna fursa za kiuchumi,atakuletea misaada na hata kuingia mikataba mitamu na wewe huku akiwa na ajenda yake kuu ya kujufaika kiuchumi!.
Unapoingia kwenye mahusiano na taifa lolote,sharti uwe na ajenda ya kiuchumi,hata uteuzi wa mabalozi leo lazima ubadilike,tunapokuchagua kuwa balozi,wewe ni ni kachero,ubalozi ni jina tu,kazi yako ni kwenda kufanya ukachero wa kiuchumi,ujue nchi yetu itafaidika vipi huko ulipo?
Hii ni sawa na hili la Jumuiya ya Afrika mashariki,uwepo wa nchi hizi ndani ya jumuiya unalenga kila nchi ipate faida za kiuchumi siyo kuungana ili kurahisisha mtanzania kufunga ndoa na Mnyarwanda!.
Bahati mbaya sana,watanzania hawazungumzi kabisa kuhusu jumuiya ya afrika mashariki,kule Nairobi,Kampala na Kigali,wenzetu hawalali wanatafiti fursa zilizomo ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki!.
Hiku kwetu,kuanzia Chake chake,mji mkongwe,Dar es Salaam,Arusha,Kigoma mpaka Mbeya,tupo kimya hatuzungumzi wala kuambiwa watanzania ajenda yetu kuu ndani ya jumuiya ya afrika masharini ni ipi?
Watanzania badi fikra zetu kwenye suala la mahusiano ya kimataifa zimefungwa na "political diplomacy" badala ya "economic diplomacy"!.
Leo si bungeni kwa watunga sera zetu,si shule za msingi mpaka vyuo vikuu kuna mjadala kuhusu ajenda ya Tanzania ndani ya jumuiya ya afrika mashariki!.
Angalau kidogo wakati wa Marehemu Mzee Samweli Sitta,kulikuwa na kampeni ya kuwaaamsha watanzania wajue nankuchangamkia fursa ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki,leo tumesinzia kuanzia mitaani mpaka vyuo vikuu,halmashaurini mpaka bungeni!.
Watanzania wengi hawana uelewa wowote kuhusu jumuiya ya Afrika Mashariki,hata sisi watu wa media tupo kimya,hatusemi chochote,watu wa jumuiya hawana program yoyote kwenye vyombo vya habari inayowaamsha watanzania kuzijua fursa ndani ya jumuiya!.
Inasikitisha,leo nenda pale Arusha zilipo ofisi za makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki,tafiti kuhusu akina nani wanashika vitengo ndani ya jumuiya,Kachunguze mwenye pale Arusha,Kenya,Rwanda na uganda ndiyo wameishika jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye utawala,watanzania wanarudi nyuma kila kukicha,wapo kama vifaranga waliokosa mama!.
Nchi wenzetu wanachama wapi kimkakati,leo wawakenya wamejaa nchini Tanzania wakikufunzi Kiswahili vyuo vikuu,wakenya nanwaganda wamejaa wanakufunzu kingereza kwenye shule binafsi,watanzania wanashuhudia tu huku wakiwa wanyonge!.
Hebu watazame Wakenya,Wanyarwanda na waganda ndani ya bunge la afrika Mashariki,wametuletea waliowahi kuwa wanasheria wakuu,mawaziri wastaafu,waziri mkuu mstaafu,Jenaral wa jeshi,makachero wabobezi!.
Hawa watu wapo kimkakati ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki,watazame wanyarwanda wanavyowekeza kwenye lugha ya kiswahili,muda si mrefu walimu wa kiswahili duniani watatoka Rwanda na Kenya,watanzania wamelala,wanabishana siasa za CCM na Upinzani tena kwa kukomoana!.
Tazama bidhaa zinavyoingia nchini kutoka nchi jirani zetu,je sisi tunaingiza nini Rwanda na Kenya?Wakenya leo benki yao (KCB) ina matawi Tanzania,ni lini NMB itafungua matawi Nairobi na Kampala?Vyuo vikuu kutoka Uganda na Kenta(Kampala International na Jomo
Kenyata)Vina matawi nchini Tanzania,lini Chuo kikuu cha Dsm kitafungua matawi Kigali na Bujumbura?
Leo vyombo vya habari vya kimataifa vinavyotangaza kwa lugha ya kiswahili,vinafungua makao yake makuu ukanda huu nchini Kenya na si Tanzania kulipo na wasikilizaji wengi!.kwa nini kenya na siyo Tanzania?
Jana nilimsikia mmoja wa wagombea wa nafasi ya ubunge katika bunhe la Afrika Mashariki akisema,"tunapotoka nje ya nchi,sisi ni watanzania na Rais wetu ni John Magufuli"ni nukuu bora kwangu,lakini je watanzania wanafahamu kwa nini tupo ndani ya jumuiya?ajenda yetu ni nini?
Je tunazijua fursa zilizopo Kampala,Juba,Bunjumbura,Kigali na Nairobi?
Watanzania wenzangu,"Political diplomacy"ishakufa,iliyopo ni "Economic Diplomacy",Hata pale chuo cha Diplomasia Dsm,Political diplomacy inafundishwa kama historia na nadharia tu iliyopata kutokea,ila Economic diplomacy inafundishwa kama mkakati unaoishi na kutekelezwa kote duniani!.
Wasalaaam na usiku mwema!.