Watanzania tubadilike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tubadilike

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Comi, Jun 20, 2012.

 1. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Watanzania wengi pamoja na kwenda shuleni,vyuoni bado wana matatizo lukuki kutokana na kuadhirika kisaikolojia,
  asilimia kuwa wanaenda kupata vyeti na sio elimu na hili ni tatizo kubwa sana na ndio maana kila leo unasikia fulani alifoji cheti na hii yote ni ili apate cheo mahala fulani.

  Tubadilike, ni heri kukosa cheti kuliko kukusa ujuzi kwani ujuzi ni bora zaidi ya hicho cheti,Je cheti ndicho kinachofanya kazi? Leo hii ofisi nyingi za serikali na binafsi customer service/care ni mbovu je , wahusika hawakupitia mafunzo? La walipitia isipokuwa walienda kuchukua vyeti.

  Yatupasa kutumia elimu/ujuzi wetu sehemu tulipo na hii ndiyo changamoto tuliyonayo la sivyo tutazidi kulalamika kuwa wageni wanaajiriwa nchini mwetu na wazawa wanaachwa.
  Penda kazi yako,furahia kazi yako,heshimu kazi yako boresha mazingira ya kazi yako kwa maendeleo yako mwenyewe,wafanyakazi wenzako,jamii yako n.k
  je utaweza kujiajiri kama utendaji wako ni mbovu
   
Loading...