Watanzania tuache kusoma hizi Course (Kozi) supply imekuwa kubwa Kuliko demand

Nasomesha chuo cha afya lakini kwa uzi huu nalazimika kubuni ujenzi wa hospitali ndogo despensary ili akitoka huko ajiajiri tu kwa upepo ulivyo, maana unatisha.
 
Wakuu,nimejitahidi kusoma ushauri wenu hapo juu nimeona una maana, sasa nina swali, je mimi niliyosoma Art O level mpaka A level ninaweza kusomea drilling ? Lengo ni kufanya kazi migodini, au hata kwenye ma project hayo mfano SGR, kwa hapa Mwanza chuo gani nitapata ?

Nataka niweke hii degree pembeni nisome vitu kama machine operator, naombeni ushauri wa chuo hasa hapa Mwanza
 
Mkuu nje ya mada kidogo, vipi unampenda sana Mo Music ee!?
 
Hayo ma course ni mpaka veta mkuu kaulizie veta mwanza utapata msaada
 
Operator wa machine nadhani ni wewe tu usomee au upate nafasi mahali ya kujifunza
Kuna jamaa alikuwa dereva naona akapata mahali pa kujifunza sasa anasukuma hayo madude
 
Sahihi kabisa
Hyo yote n kwasababu ya kukosa muongozo pnd tunapokua masomoni tunaona yote sawa tu ilimrad nyumban wanajua tupo chuo kikuu mwsho wa siku inabd turud vijiweni tu na muda wote tuliopoteza ni sawa na bure mm nawaza niende tena veta nikajifunze ufundi
 
Watu wote wakiwa mainjinia sijui itakuaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…