Watanzania tatizo la Tanzania ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tatizo la Tanzania ni nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by pansophy, Nov 22, 2011.

 1. p

  pansophy JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Tanzania ina rasilimali lukuki ingawa bado tu masikini wakutupwa, tunabembelezwa kwa kuambiwa uchumi wetu unakua kwa kasi ingawa faida haionekani kwa sisi Watanzania wa kipato cha chini tulio wengi. Tatizo haswa ni nini, ubinafsi(rushwa),kutokuwa wazalemdo,ujinga(lack of education) au.......?? Tuelimishane wapendwa
   
 2. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Tanzania inavyote isipokuwa watanzania.
   
 3. p

  pansophy JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Sasa sisi wakina nani?
   
 4. M

  MyTz JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  uoga wako wewe na wenzako...
   
 5. p

  pansophy JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mytz wewe umethubutu? Au na wewe ni walewale Wakwere. To dare is to do mpwa
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Na kwanini unabaki kuwa Mtanzania wa kipato cha chini? kuna fursa chungu nzima za kukufanya ujiendeleze kwani unangoja uletewe mifuko ya fedha?

  Sasa hivi unafanya kazi ipi? una kisomo kipi? unaishi wapi? una umri gani? nijibu hayo maswali nikupe mawazo ya kukutoa kwenye kipato cha chini.
   
 7. p

  pansophy JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Naona wanichimba, nazungumza kwa niaba ya Watanzania walio wengi. Bk to me ni self employed kwenye IT industry, pia nimebahatika kupata MSc SBIT. Ntashukuru msaada wako Mh FaizaFox
   
 8. mpoleeee

  mpoleeee JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kipato cha chini kinachangiwa na kukosa maujuzi.
   
 9. p

  pansophy JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Sasa 2tajikomboaje, maujuzi yatakujaje? Radio nyingi channel chache. Wengine 2namaujuzi but hatupendi kulaliwa, elimu haiozi
   
 10. libent

  libent JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hilo swali aliulizwa mzee wa kaya a.k.a baba riz huko ughaibuni akajibu nae hafahamu kwa nini watanzania ni maskini
   
 11. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160

  Naomba unipe maujanja sister. Nipo wilaya ya Siha, Kilimanjaro. Nina 1st degree ya social science na Ms degree ya Enterpreneurship zote za Mlimani. Nimemaliza mwaka jana na hadi leo sina kazi hadi sasa! Nimetuma application hadi nimeishiwa. Wazazi ni wakulima na hawana uwezo wa kunipa mtaji. Nifanyeje?
   
 12. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  kuna simulizi kuwa 'mzungu' wa kwanza kufika Mwadui alikuta wananchi wa pale wanacheza bao (?) kwa kutumia almasi na ndio akawaahidi kuwaletea 'kete' nzuri zaidi endapo wangemkusanyia almasi zaidi, then akawaletea za plastic.
  kama umewahi kusoma hiyo 'story' ambayo inafanana na nyingine nyingi, jiulize ni miaka mingapi imepita na ni mabadiliko gani yametokea kwa hawa watu na vizazi vyao!? Je, haifanani na mtu anayechukua suti kwa kubadilishana na mbuga za wanyama? ...land cruiser kwa kubadilishana na shirika la ndege? ...nyumba (ghorofa moja) kwa kubadilishana na hekta 700,000 za ardhi yenye rutuba?
  Ukipata majibu ya haya maswali then uangalie kuanzia wakati huo ni watu wangapi walikuwa hawana elimu na sasa wamesoma (graduates/doctorates), na ujue kuwa Watanzania tulio wengi kila siku tunaamka na kwenda 'kazini' lakini mambo ni yale yale!
  Suluisho ni sote kuwa na vision ...kama mtu mmoja mmoja na baadae tuziunganisha ziwe za group zima la Watanzania (za pamoja).
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Dada faiza bado nakusikilizia!
   
Loading...