Secret Star
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,720
- 1,639
Leo nijaribu kuzungumzia kuhusu hili suala la kitengo cha uhamiaji, hapa Nchini.
Ni wazi kuwa wazungu kwa asilimia kubwa wanatuibia mno, Hili najua kila mtu anatambua, kwa hali hiyo naamini watu wengi walipaswa kuwachukia Wazungu na kuwaona kama ni maharamia siku zote, Ila cha kushangaza, hali ni tofauti kabisa!!!,
Mbali na kwamba wazungu wanaiba ila wanaendelea kupendwa mno, isitoshe wanapewa fursa na nafasi za mbele zaidi kuliko hata tunavyojipenda sisi wenyewe!
Ni kiasi cha Miezi miwili sasa, Ndugu zangu kutoka Norway, Oslo walituma maombi yao ya kupata Visa, ili waje huku Tanzania kwa shida binafsi, kwa muda. Na hapohapo wanapoishi nyumba kama ya nne pia kuna wakorea ambao walihamia Norway pia walituma maombi hayo ya Visa, wote kwa siku moja kwenda Stockholm, Sweden kwenye ubalozi wa Tanzania kule SCANDINAVIA....
Baada ya muda kama wa siku mbili waliletewa feedback kuwa maombi yao yalikuwa yameshafika Sweden, na walipopiga simu Sweden waliambiwa kuwa maombi hayo yalifika na kwamba wao walishayatuma Tanzania, kwa ajili ya ruhusa,
Muda ukaanza kwenda, na kiasi cha wiki nne za kwanza zikapita ambapo jambo la ajabu wale wakorea walikuwa wameshatumiwa Visa! Ila hawa weusi hawa wao walipowapigia simu Ubalozini Sweden wakaambia kuwa bado maombi yao yalikuwa hayajajibiwa kutoka Tanzania!
Wiki moja baadae kimya wiki mbili kimya wiki ya tatu kimya sasa hivi tunasubiri wiki ya nne itimie na maombi hayo bado idara ya Uhamiaji Tanzania imekaa kimya! Na hao ndugu si mara yao ya kwanza kuja huku!
Sasa nawashangaa mno ndugu zangu waTanzania yaani ni kweli kwamba wapo radhi wampe Visa mtu mweupe na mweusi mwenzao wamnyime! Yaani wampe huyo mweupe ili aje aendelee kutuchorea ramani za kutuibia!
Mweusi mwenzao Ndugu yao wamchinje, upande wa pili waendelee kukaribisha wezi! Kweli kwenye akili zetu weusi tuna nyingine za ziada ambazo sio za kawaida...