Watanzania sasa hatuko salama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania sasa hatuko salama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mayoscissors, Oct 18, 2012.

 1. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Wana Jf,
  Watanzania tunapenda kusononeka pale mambo yanapoharibika na baada ya muda mfupi tunasahau na kusonga mbele na mizigo yetu ya maisha yasiyo na matumaini.
  Sakata la ufisadi,migomo ya madaktari na waalimu,mateso kwa doctor ulimboka,kuuwawa kwa hayati Daud Mwangosi na polisi,kuuwawa kwa wafuasi wa vyama vya siasa,kuuwawa kwa APC Barlow,kuuwawa kwa coplo saidi zanzibar na sakata la watanzania wenzetu waislamu kuchoma na kuharibu nyumba za ibada ya watanzania wenzetu wakristu ni mambo yanayoashiria kuwa si mbali ukabila na udini ambao tz tumekuwa tukisifiwa kuwa tumefanikwa kuondoa maadui hao sasa tumeyarudia matapishi ambayo yatatufikisha pabaya.
  Binadamu tuna asili ya ubaguzi ila ustaarabu ndo umefanikisha binadamu wengine kuthibiti hali hii.Rai kwa watanzania wenzangu tuwe na uzalendo na tuishi kwa umoja wetu kama watanzania na tuweke pembeni tofauiti za imani na ukabila kwani si mbali tutatumbukia kwenye wimbi la mauaji kama wenzetu Rwanda ambao leo wanajutia unyama huo waliofanyiana kama mahayawani.
   
Loading...