Usishange kuona watu wanahangaika kupanda madaladala kwenda kazini ama wengine wanatembea kuwahi kazini. Suala hapa ni hivi; watu hawa hawa wanaowai kwenda kazini wakifika huko hawafanyi kazi, wao ni domo tu, umbea, kuperuzi wasanii feki (bongo fleva) wamefanya nini jana ili wawaige wakiwa kazini, ukienda ofisini mwao kufuata huduma hakun wa kukusaidia. Cha kushangaza ukifika huko ofisini kufuata hiyo huduma utakuta watu kila mmoja kwenye computer akiperuzi wasanii wa marekani wanafanya nini. Utakaa unasuburi, ukiuwauliza utawasikia subiri niko bize.