Watanzania ni Mazombi kiasi gani?

Watanzania ni Mazombi kiasi gani?

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
Anaandika Malisa GJ

Ripoti ya CAG ya mwaka 2015 (wakati wa JK) inaonesha deni la matibabu nje ya nchi kwa watumishi na viongozi wa serikali kwa kipindi cha June 30 hadi December 31 mwaka 2015 liliongezeka kwa Sh.Bilioni 2.25 kutoka Sh. bilioni 16.94 hadi kufikia Sh. bilioni 19.19. Kwa Lugha rahisi ni kuwa ndani ya miezi sita (June 2015 hadi December 2015) viongozi wote waliotibiwa nje walitumia shilingi Bilioni 2.

Serikali ya JPM ilipoingia madarakani ikasema gharama hizo ni kubwa. Hivyo ikazuia matibabu nje ya nchi, hadi kibali maalumu. Mwezi April mwaka juzi Spika Ndugai akasema "ili wabunge kupata matibabu nje ya nchi ni hadi Rais atoe kibali". Hii yote ni katika kubana matumizi na kuzuia viongozi kwenda nje hata kwa magonjwa yanayoweza kutibiwa nchini.

Kwahiyo wananchi walitegemea gharama za matibabu nje ya nchi zitapungua mara dufu. Kama mwaka 2015 zilitumika Bilioni 2 kwa miezi 6 zikaonekana ni nyingi, basi baada ya zuio hilo zingetumika fedha kidogo zaidi.

Lakini mwaka jana zimetumika mara dufu ya awali. Ripoti ya CAG inaonesha kuwa katika kipindi cha June 30 hadi December 31 mwaka jana deni la matibabu kwa viongozi nje ya nchi limeongezeka kutoka shilingi bilioni 28.6 mpaka shilingi bilioni 45.7, sawa na ongezeko la shilingi Bilioni 17.1 za kitanzania.

Kwa lugha rahisi ni kuwa ndani ya miezi 6 tu kwa kipindi cha mwaka jana serikali ilitumia Bilioni 17.1 kwa matibabu ya viongozi nje ya nchi.

Swali la msingi ambalo wengi wanajiuliza ni akina nani waliotibiwa kwa Bilioni 17.1 kwa miezi 6 tu? Kwa kuwa serikali imezuia viongozi kutibiwa nje bila kibali maalumu (cha Rais) tulitegemea gharama zipungue sana, lakini badala yake zimeongezeka maradufu. Kwanini?

Je kuna watu wanakwenda nje kutibiwa kimyakimya bila taarifa zao kuwekwa wazi? Kama wakati wa JK Bilioni 2 kwa miezi 6 zilionekana nyingi, kwanini mwaka jana imetumika Bilioni 17.1 na serikali ipo kimya?

Angalau wakati wa JK tuliona watu wakienda nje kutibiwa mara kwa mara, kwahiyo kutumia Bilioni 2 kwa miezi 6 was very possible. Lakini sasa hivi watu hawaendi nje kwa matibabu na bado zimetumika Bilioni 17.1. Ni ngumu kuingia akilini.

Bunge letu dhaifu limekataa kufanyia kazi ripoti za CAG. Hii ina maana kuwa ufisadi kama huu utafunikwa.

Kama bunge lingekuwa imara lingeifanyia kazi ripoti ya CAG kwa kuibana serikali ieleze ni kwanini gharama za matibabu nje ya nchi zimeongezeka maradufu, wakati idadi ya wanaoenda kutibiwa nje imepungua. Kama hata Lissu walikataa kumtibia, inakuaje gharama ziwe kubwa hivi? Ni akina nani hao wanaotibiwa kimyakimya kwa mabilioni?

Haiwezekani Bilioni 2 kwa miezi 6 wakati wa JK ionekane ni matumizi mabaya ya pesa, halafu Bilioni 17.1 kwa miezi 6 kipindi cha JPM ionekane kawaida.

Lingekuwepo bunge imara la Sitta ama Makinda tayari ingeshaundwa kamati teule ya kibunge kuchunguza swala hili. Na ripoti ingesomwa bungeni kwa mbwembwe na kama kuna harufu ya ufisadi wahusika wangeshughulikiwa. Lakini kwa bunge hili dhaifu linaloongozwa na Bwana Spika dhaifu sana, expect nothing than business as usual.!
 
Kumbe.. Sisi tunapoenda shule tunaenda na medical examination sasa ni zamu ya wabunge wakigombea walete medical examination zao ili mgonjwa abaki nyumbani mzima afanye kazi
 
Haya mambo kuweza kuyahoji awamu hii inabidi uwe na moyo kama wa Lissu, ama imani kama ya Kinjeketile.
 
yeye mwenyewe hayoo mabilioni anayatumia sanaa. Hawezi kuruhusu serekali ibanwe.

Africa tunasafari ndefuu sana kuendelea.
 
Back
Top Bottom