Watanzania na misitu yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania na misitu yetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by broken ages, Apr 12, 2012.

 1. broken ages

  broken ages Senior Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 160
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Nionavyo tunapaswa ama kuangalia upya sheria inayolinda maliasili zetu kama misitu na tunapaswa kuweka uzalendo sana ktk hili.kuna ukweli kwamba serikali ya Kenya imepiga maruku uvunaji wa aina yeyote ya miti katika nchi yake ama ndani ya aridhi yake lakini maruku hayo hayaandamani na uzuiaji wa matumizi ya mbao ama bidhaa za miti, na inavyosadikika ni kwamba kwa sasa Kenya inatgemea zaidi mazao ya miti ama mbao zaidi kuiport kutoka TANZANIA.je serikali ya Tanzania haioni hatari ktk hili? Kuna sababu gani ya kuweka usalama wa taifa kwenye mipaka iwapo bidhaa ama rasilimali za taifa kama hizi zinaweza kuwa zinapita tu na wala hao usalama wa taifa wasione ama wasichukue hatua ya kuishauri serikali kuzuia hili?ama Tanzania tuna misitu mingi zaidi kiasi kwamba hata ikivunwa na kusafirishwa nje haitakuwa na athari kwa nchi?ama kweli tunakuwa wavivu wa kutambua na hata vipofu wa kuona haya yote yanapotendeka? Maswali haya yote na mengi mengineyo nimekuwa najiuliza bila kupata jibu la kutuliza akili yangu mwanajf naomba tubadilishane mawazo ktk hili.
   
 2. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,535
  Trophy Points: 280
  Upigaji wa marufuku hautasaidia sana kama hakuna utunzaji mzuri wa misitu. Utunzaji ambao utazingatia kwamba,watu waishio kando ya misitu wanaona na kupata faida ya utunzaji huo. Utunzaji ambao utazingatia kwamba,hakuna wajanjawajanja ambao wanafaidika kuliko wenzao katika ngazi ya kijiji. Utunzaji ambao utazingatia kwamba kuna mgawanyo sawa wa faida na hasara,hususani pale panapokuwa na utunzaji shirikishi,baina ya dola na wanajamii waishio kando ya misitu. Utunzaji ambao utazingatia kuepuka kurudisha mfumo wa zamani wa utunzaji wa misitu "fortress/fences and fine conservation",ambao ulikuwa ukiwaona wanajamii waishio kando ya misitu kama tishio kwa uwepo endelevu wa misitu;mfumo ambao mabwana misitu walionekana kama mapolisi,na walitenda vitendo vya kinyama kwa wanajamii waliokuwa wakikutwa misituni n.k.

  Kwa kuzingatia hayo na mengine mengi ambayo yameshaandikwa sana na watafiti wa masuala ya misitu,hakika Tanzania haitakuwa na haja kuiga walichofanya Kenya.
   
 3. M

  Mgalatia JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 28, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tutaendelea kutafuta visingizio kama kawaida yetu na baada ya miaka 10 tutaendelea kuwa ombaomba tusaidiwe kuanza kupanda miti. Mfano Moshi kumekuwa na joto Kali sana, pengine ni kwa sababu ya uvunaji wa misitu. Ajabu kabisa mtu mmoja amenieleza kuwa wanapanda miarobaini huko milimani! Naona kuna mambo ya kiabunuasi yanaendelea kwetu na si ajabu jirani zetu wakawa wanatucheka.
   
Loading...