Watanzania na milango ya maduka too much | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania na milango ya maduka too much

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by nunu, Aug 17, 2012.

 1. n

  nunu Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Katika pitapita za hapa jijini na hata huko mikoani kunakasi sana ya kila jengo kuwa na milango ya kukodisha maduka. Maana yake ni kuwataifa limejipambanua kama wachuuzi wa bidhaa za ndani na nje. Hizi za nje maanayake ni matumizi ya dollar ambazo uwiano wa kuingiza dollar na kuzitumiakuagiza bidhaa si mzuri. Lini tutajengania na uwezo wa viwanda vidogo vidogo, vya kati na vikubwa?

  Tukililea hili litakausha hata akiba ndogo ya dollar zetu kwa uchuuzi wetu. Muhimu tutengenezebidhaa tuuze nje tupate dollars. Je hatua zipi zichukuliwe ukizingatia sera za biashara ni nzuri tu??
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  People are looking for ways to make ends meet my friend...
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mazingira bado hayaruhusu kuwekeza kwenye hivyo viwanda kwa sisi wazawa. Kwanza umeme bei juu, maji bei juu, miundo mbinu ndio hivyo tena hamna usafiri wa nafuu kwakuwa Reli zote mbili zimekufa. Tumebakia kubebesha mizigo kwenye mafuso na kodi nazo hazieleweki. Bado huo mzigo kama ni malighali etc haujasimamishwa barabarani kila Traffic Police akiona mzigo wa business anataka chochote japokuwa documents zote zipo.

  Huko kwenye kutafuta vibali nako ndio usiseme afadhali akija Mzungu/Muhindi/Mwarabu hata huko kwenye kutafuta vibali serikalini watamnyenyekea kuliko sisi kwa sisi wenyewe ngozi nyeusi. Waki consider haya yote watu wanaona bora wanunue viti 2 vya dentist na mashine 2 za kunyolea au waende China wakalete FONG KONG!
   
 4. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 847
  Trophy Points: 280
  Ubunifu hatuna! Ukiona mwenzio katoka kwa style ya duka nasi tunafata huko huko! Tunahitaji mabadiliko kwa wenzetu wana shopping malls sisi bado hatujafika huko, lakini kwa hili somehow linatusaidia meaning uchumi unabaki kuwa wetu na mtaji unaoweza kuwekeza ni mdogo.
   
 5. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2012
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,562
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  You nailed it buddy
   
Loading...