Watanzania na mapokeo

Watanzania na mapokeo

MWANAUME UGOKO

Senior Member
Joined
Nov 4, 2017
Posts
122
Reaction score
235
Habari wanajamii,natumai Jehova wetu ametupa tena nafasi ya kuiona siku hii hivyo tumshukuru.Nami kwa mara ya kwanza nimeamua kuandika hii habari kutokana na kuendelea kuwapo kwa kundi kubwa la watu waaminio mambo mbalimbali kutokana tu na mapokeo,simulizi na kuyafanya kuwa kweli ilhali si kweli.Tabia hii imejijenga vichwani mwa watanzania wengi na kuwafanya waamini hivyo bila ya kuwa na uhakika,mfano mwepesi ni katika siasa na maisha.

Nchi hii ni vyepesi kumkaririsha mtu uongo na ikachukua muda sana kumkaririsha ukweli moja ya mambo ama mapokeo waaminio watanzania kwa nguvu zote ni

1: ughaibuni kuna maisha ya raha na starehe nyingi kwa jasho kidogo

2:Mjini kuna maisha mazuri kuliko kijijini

3:Maendeleo huwa ni kama zari tu

4:Vyama vya upinzani ndo waliobeba kapu la asali na maziwa

5:bila ya ccm nchi itaanguka na mengine mengi.Nilishangaa sana kukuta Kilimanjaro Magufuli (jiwe) anakubalika na wachaga walio wengi kuzidi hata kanda zingine,na kwa muda niliokaa kaskazini babati,arusha,machame,himo na kirua ulinipa kujifunza kitu kipya na kigeni.1995 Augustine Mrema akiwa mgombea urais gari lake lilisukumwa na wananchi jijini mwanza kwa mapenzi yao na kubadili sura ya siasa miaka hiyo,hili jambo lilifanyika kanda ya ziwa kwa nini hakufanyiwa kaskazini?.

Pia kumekuwepo na mapokeo ya kuamini mjini ndo kila kitu na kutengeneza kundi kubwa la watu wakimbiliao mjini na kuacha maisha mazuri kijijini,wakienda kuishia kuwa mateja vibaka kisha huzeekea katika maisha ya upangaji na yenye shida kubwa,baadhi ya maisha ya watu walio wengi mjini ni taabu na dhiki kuzidi hata kijijini na hata muonekano mitaa mingine inaonyesha sura ya shida na dhiki hasa majiji yetu matatu dar,mwz na Arusha(ukiondoa yaliyowekwa kisiasa).mitaa kama keko mwanga(dar) mabatini(mwz) unga ltd,ngarenaro(Arusha) vingunguti manzese buguruni(dar) butuja nyakabungo(mwz) hali ni duni kuliko hata kijijini hivyo kujenga uhalisia wa maisha halisi na si mapokeo.

Rafiki yangu mmoja yuko Afrika kusini alikojiripua alifiwa na mzazi wake akawa hana hata ile nauli ya kuja bongo msibani.pia kuna rafiki yangu mkenya nilikuwa nae mwanza 2006 kipindi kile cha mfumuko wa wasanii kila uchochoro akitafuta kutoka tukiwa wote Mo records,alifanikiwa kwenda USA 2009 mpaka dakika hii hajawahi kukanyaga kwao.Je mapokeo hujengwa na nini? ¡,ukosefu wa elimu ¡¡, kupumbaa kwa akili,na moja ya pokeo linaloitafuna jamii ni kuwaamini wanasiasa kuwa ndo nguzo kuu na hatima ya maisha yao ya usoni kuelekea nchi ya ahadi,kwani kunapishana nini kati ya utawala wa kikoloni na tawala za dunia ya sasa?

Wakati wa ukoloni wanasiasa walifungwa na kuuliwa,walishitakiwa kwa uchochezi,kulikuwa na shule za walio daraja la juu na shule za akina kayumba,polisi wa kikoloni waliua watu na kuzuia mikusanyiko mfano ni mauaji ya soweto,wakoloni walikataa kukabidhi madaraka.Mapokeo ndo yamedumaza maendeleo yetu,katika dunia hii mwamini askari aliye mstari wa mbele vitani akiipigania nchi yako na si mwanasiasa,kiongozi wa dini au mtu yeyote kwani hutanguliza maslahi yake kwanza mbele.
 
Somo zuri, but what's ur concept?
 
sawa ila siku nungine kumbuka hata kuweka aya basi maana huo uandishi si mchezo
 
Back
Top Bottom