Watanzania Na Dhana Ya Ukiritimba wa Kikoloni Ubongoni mwetu.

tzfanatic

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
626
382
Ndugu Watanzania Wenzangu na Wana Africa Ya Mashariki habari za Masiku Tele, Nina Muda Mrefu sana Sijaleta Uzi wenye manufaa zaidi Ya jokes ili kuwekana Happy sometime. Kuna Jambo moja muda mrefu lanitatiza sana Ndani ya kichwa changu na Hasa juu ya upeo wetu watanzania sina uhakika na kwengine balani africa ila kwa fikra zangu yakinifu naona kabisa kwa kiasi kikubwa tunafanana kimawazo na kifikra.

Sina Miaka Mingi dunia Kiasai cha Kufika Madahari ila ni nimekuala chumvi kiasi chake kuweza kupembua na kuyaona haya.

Natatizwa na fikra hizi mfu hasa za wanaojiita wasomi, kusupport kauli ama matendo au, Jamii ya watu wa bara hili pendwa lenye kila nakshi, Hakika alieyumba mbingu na ardhi amelijalia. Unamkuta Msomi ama Kijana ambaye kifikra unaona ama unahisi anajitambua, akiongea maneno yasiyo na tija kwa jamii yake na hata kumkufuru aliyemuumba kiasi ya kwamba akiona kama amekosea kumpa rangi nzuri na kumweka mahali palipo na utulivu.

Hakika ukoloni umetuhathiri sana kiasi ya kwamba tunashindwa jielewa na hata kupanga mambo yetu, na kushindwa kupiga hatua stahiki, wametuvuruga kiasi ya kwamba wenyewe kwa wenyewe hatupatani , hatuelewani na wala hatujui nini tunataka , WAMETUFANYA TUMEKUWA TEGEMEO KWAO NA TUWE NA DHANA KUWA WAO NDIO KILA KITU. Hakika hapa tumepotoka sana.

Leo hii mzungu ama mtu mweupe yeyote anaonekana anathamani, kuliko yoyote ....mfano leo hii waafrika na watanzania akitaja israel mishipa ya shingo itamtoka kutetea na hata kuwaita taifa teule la mungu, hakika wamefanikiwa,...

Sisemi ni makosa la hasha inaweza kuwa la kiimani, lakini je kwanini unashindwa kutumia simple logic ya kuweza kujiuliza, ina maana we si mteule, kama yeye ndiye je wewe umeumbwa kwa sababu gani?,.

Nimalize kwa kusema Africa yetu ili iendelee, katu hatutakiwi kukopi kutoka kwao bali ,tunatakiwa tuwe na mfumo wetu , wenyewe kama walivo asia na ulaya.

Kila nchi inabidi iwe na vipaumbele ambavo ni endelevu na kila raisi anayeingia, basi ahakikishe anaondoka vimetimia , na kama akishindwa basi mfumo umkatae na ajibu kwanini kashindwa...

hakika waafrica ni wamoja na kama tukiamua na tukishirikiana kweli hakuna wa kutushinda......
 
Back
Top Bottom