Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,181
- 1,579
Wakati mtu anaenda kulala usiku; atakuwa ni mpumbavu tu endapo ataacha mlango wazi maadamu tu amemwomba Mungu amrinde!
Mimi Sijui kama imani ya namna hiyo ipo!
Na kama ipo, basi, hiyo ndiyo dini ya mashetani tunayosikia habari zake.
Kwa kuwa ni shetani tu mwenye hurka ya kumjaribu Mungu!
Katika nchi hii tumekuwa na viongozi wa kidini, na wa kisiasa wa ajabu sana!
Watu hawa kwa muda mrefu; macho yao yamekuwa yakiiona hatari wakati wa uchaguzi tu na si vinginevyo.
Wakati huo ndipo utawasikia wanatuambia kwamba iombeeni nchi yetu ili ipite salama katika kipingi hiki
Huku tukishuhudia mikesha, dua, na sala kila mahali. Ndiyo sikatai hiki tukifanyacho kina nafasi yake, lakini pamoja na hayo kama taifa viongozi wetu walipaswa kutumbia umuhimu wa kuifunga milango ya nyumba yetu inayoweza kuipenyeza hatari mpaka ndani.
Mimi daima nimekua najiulliza bila jawabu!
Je watu hawa ni kweli hawafahamu kama nyumba yetu milango yake iko wazi?
Tazama!
1) Kuna mlango wa kukosekana kwa tume huru ya uchaguzi.
2) Kuna Mlango wa uminyaji wa makusudi wa demokrasia.
3) Kuna Mlango wa matumizi mabaya ya vyombo vyetu vya usalama wakati wa uchaguzi wenyewe.
Milango hii tulipaswa tuifunge kwanza halafu ndipo tukumbushane sote kuomwomba Mungu kabla ya shughuri yenyewe.
Tofauti na hapo maombi yetu yatakuwa bure, tena tutaonekana tunamjaribu Mungu tusipofunga milango kabla ya uchaguzi.
Na kama tutaendekeza tabia hii mbaya hatari itaingia tuu!