Kuna mcatholic aliwahi kuandika kitabu chenye jina la wacatholic mnakichaa?
alikuwa amehama dini flani na kuingia kwenye ucatholic.
Leo na mimi naomba niwaulize watanzania(au angalau watanganyika) mnakichaa!?
Hivi ndivyo mataifa au mgeni yeyote akija Tanzania atajiuliza na pengine wajukuu wa wajukuu
wetu watajiuliza, ni kweli tulikuwa na kichaa kwa ujumla wetu!?
Kuna mtu mmoja alipata kusema hakuna kitu cha kipumbavu sana kama kumpa mtu au watu madaraka
ambayo huwezi kuwawajibisha au hawatawajibika kwa chochote watakachofanya.
Magufuli alitumia loophole hiyo,
kikwete alitumia loophole hiyohiyo,
Mkapa alitumia loophole hiyohiyo,
Mwinyi alitumia loophole hiyohiyo,
Nyerere alitumia loophole hiyohiyo,
Na sasa Samia anatumia loophole hiyohiyo,
Na mwingine atakuja atatumia loophole hiyohiyo.
na wao wanakili hilo kikwete alinukuliwa akisema ukiwa raisi na mwenyekiti wa CCM unakuwa
na nguvu sanaaa!!!, hakumalizia tu kuwa ukiwa hakuna mtu wa kukuwajibisha.
Hili halihitaji maono kuvuviwa na roho wa bwana au malaika kukuonyesha kwenye njonzi.
tutegemee viongoz wa aina hiyohiyo mpaka pale tutakapo weza kuwawajibisha
hao tunao wapa madaraka kwani madaraka yanalewesha hasa kama huta wajibika
kwa chochote utakachofanya bali tu nafsi na utashi wako utakavyo itakavyo kutuma.
Magufuli alichokifanya cha tofauti mpaka kupigiwa kelele sana ni kuwa gusa watu
wa chama chake na pengine watu wa nje wenye maslahi yao Tanzania.
Madelu anajua hatawajibiuka kwa chochote atakacho fanya, february anajua hatawajibika
kwa chochote atakachofanya, jaribu kuwaza wewe ungefanya nini kama ungejua hutawajibika
kwa chochote utakachofanya hata kwenye maisha yako ya kila siku!?
Njia pekee ya kufanya ni kuwawajibisha hawa watu, sio kulalamika, sio kulia lia,
sio kusubiri huruma yao la hatuwezi tukae kimya tuendelee kuwa vichaa angalau itasaidia
kilo kupoteza mda na nishati kama kelele za chura kwa tembo anayekunywa maji.
nb: Tanzania haijawahi kupata raisi kichaa ila watanzania wenyewe ndio wanakichaa,
Msiniulize mimi nimefanya nini angalau mimi nimehamia burundi kama madelu alivyotutaka.