Watanzania milioni 13 wanakwepa kodi-Utafiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania milioni 13 wanakwepa kodi-Utafiti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Oct 1, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Aziza Athuman na Minael Msuya

  WATANZANIA milioni mbili kati ya milioni 15 wenye uwezo wa kulipa kodi ndio wanaojitokeza kutekeleza wajibu huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya Kusini na Mashariki ya AFrika (ESAURP), Ted Maliyamkono, amesema.

  Maliyamkono aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na taasisi hiyo, kujadili suala la kodi.

  “Tanzania ina zaidi ya watu 15 milioni, wenye uwezo wa kulipa kodi, lakini ni watu milioni mbili tu ndiyo wanaolipa kodi,”alisema Maliyamkono.

  Alisema utafiti umeonyesha kuwa kukosekana kwa elimu kuhusu umuhimu wa watu kulipa kodi, ni moja ya sababu zinazowafanya wengi kukwepa kodi.

  Mkurugenzi huyo alisema pamoja na mambo mengine, tatizo hilo linawafanya watu wasijue kuwa kukwepa kulipa kodi, ni kosa kwa mujibu wa sheria.

  Alisema Watanzania wengi, wanaona kuwa kulipa kodi ni uonevu na taasisi zilizoundwa kufuatilia kodi zimeanzishwa kwa maslahi ya wachache, jambo linalowafanya wafanyabiashara wengi, kugoma kusajili biashara zao.

  “Wananchi hawajapata elimu ya kutambua kuwa ulipaji kodi ni muhimu na wala hawatambui kuwa kukwepa kulipa kodi ni kosa kisheria,”alisema Malyamkono.

  Akizungumza katika semina hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, aliuomba Umoja wa Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, kuweka mazingira mazuri yatakatowavutia watu kulipa kodi.

  Alisema Tanzania imeathirika kiuchumi na kwamba sasa ni wakati muafaka kwa wananchi kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari, ili nchi ipunguze utegemezi kwa wahisani.

  “Utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari ni njia pekee ambayo inaweza kusaidia nchi yetu kujitegemea, na kuondokana na hali tuliyonayo kwa sasa ya kuwategemea sana wahisani,”alisema.
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  My take on this:
  1.Watu wanaona kodi yao inavyotumika vibaya.Mara watu wameiba kodi hiyo ( TRA iliibiwa mabilioni ya fedha za walipa kodi hii karibuni), mara zimetumika kwa matumizi yasiyo na faida ya moja kwa moja kwa wananchi kama kununulia mashangingi,n.k.

  2.Pale unapokosa huduma muhimu kama barabara, maji safi, umeme, vifaa mahospitalini na mashuleni, matunzo kwa wasiojiweza ikiwemo wazee na watoto yatima huwezi kuvutika kulipa kodi.

  3.Uhamasishaji uendane na vitendo kuonyesha kuwa kweli kuna manufaa kulipa kodi.Wengi wetu tunajua kuwa serikali inategemea kodi kuendesha shughuli zake na hivyo ni muhimu kulipa kodi!

  4.Wale wote waliohusika kutumia vibaya kodi za wananchi waadhibiwe mara moja na kutangazwa kwa wananchi waliowaibia ili liwe onyo kwa wengine.
   
  Last edited: Oct 1, 2009
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  naona kajijibu mwenyewe. Watu hawataki kulipa kodi kwa sababu hawaoni matunda yake.
  Mfano mzuri angalia hii thread by Invisible:
  https://www.jamiiforums.com/jamii-photos/40008-get-the-message.html#post599850
   
 4. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mi hapo kwenye watu milioni 15 ndio wanatakiwa kulipa kodi bado sijamuelewa.. maana kuna ile ishu ya kulipa indirect kwani unapo nunua kitu bei yake ina VAT inclusive kwa maana nyingine mtu unalipa kodi...maana kwa mkulima akiuza mazao yake anakatwa kodi sa hiyo idadi ya M15 bado sijaijua vizuri labda mnifahamishe maana kati ya hoa M3 nadhani M2 inaweza kua ya wafanyakazi wenye ajira za kudumu....
   
 5. K

  Kekuye Senior Member

  #5
  Oct 1, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata wananchi wakipewa elimu ya umuhimu wa kulipa kodi kama hatujaandaa mifumo thabiti ya ukusanyaji bado haitasaidia. Utafiti huu ni mzuri lakini vilevile ni vyema kuangalia makusanyo halali hufanyika kiasi gani na kama huwasilishwa kwa kiwango kilichotarajiwa. Inawezekana pia wakati wa kukusanya kodi makubaliano hufanyika ili mlipaji alipe pungufu na mkusanyaji akazitia mfukoni mwake bila kuziwasilisha kunakohusika.
   
 6. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Watanzania wanalipa kodi nyingi sana!. Kodi ya mauzo sales tax iko juu sana kila mtanzania analipa kodi kwenye vitu wanavyonunua mafuta, chakula, fine, vifaa vya ujenzi n.k. Siyo lazima watu wengi walipe Income tax ndiyo wawe wanalipa kodi!!. Mimi kwa mawazo yangu mfumo wa kodi ni mzuri kwani unalipa kutokana na unavyotumia. Ni bora pesa nyingi ikae kwa watu kuliko kwa serikali kwani serikali ikilazimisha watu walipe kodi wakati vitu vingi vinavyotoka nje ya nchi vina kodi kubwa itakuwa vigumu kufanya biashara bongo.
   
 7. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Pia, wakawaelemishe wawekezezaji umuhimu wa kulipa kodi!
   
 8. Panga la Yesu

  Panga la Yesu JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2009
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aleluya!
  Kwa mtazamo wangu ni kweli kila mtu analipa Kodi lakini kuna wale watu wa mwisho wanaopaswa kupeleka hiyo Kodi Serikalini ndio hao wasio lipa hiyo Kodi Serikalini.Yaani ni kusema hao millioni 15 ndo wanatakiwa kujulikana na TRA, Mkulima ahitajiki kufika TRA ila yeye anailipa kwenye Pembejeo, mafuta na vyakula na matumizi yake ya kawaida. na hii aimanishi kwa mimi ninaye takiwa kulipa Kodi TRA kwenye biashara zangu nimempunguzia mtumiaji kwa sababu mimi sitalipa la, hivyo ujue kuwa ninakula dhuluma ya wavuja jasho wengi ambao wanategemea kwa mimi kulipa Kodi yao niliyoikusanya Huduma za Jamii ziwe nzuri.

  Jambo hili linauma sana kwani ni dhambi kubwa sana, bwana Yesu alisema ya kaizari mpe kaizari na ya Mungu mpe Mungu. na hasa sisi tulio na ufahamu tunapo amua kulipa kisasi kwa kutotaka kulipa Ushuru wa kile tunachopaswa toa.
  Nchi imeingia kwenye laana kubwa na ndiyo sababu leo hii nchi inaendelea kuoshwa kwa sababu hatutimizi mpango wa Mungu. Ni wakati watanzania umefika sasa tutubu sana kwa haya yote tuliokwisha fanya.

  Mungu awabariki sana na awape ufahamu wakuelewa hili.

  Aleluyah!
   
Loading...