Watanzania lini tutaacha unafiki?


Zipuwawa

Zipuwawa

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2010
Messages
3,051
Likes
96
Points
145
Zipuwawa

Zipuwawa

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2010
3,051 96 145
Kutokana na kusoma habari nyingi za Tido Mhando kufika ukomo katika chombo cha habari cha TBC nimeona mengi sana wapo wengi waliomsifu kwa jitihada zake na utendaji wake mzuri katika kipindi chake chote cha mkataba wake.Na wapo wengi wamesema katika maoni mbalimbali kuwa Tido halikuwa hana mchango wowote ule.

Nimesema Watanzania lini wataacha UNAFIKI ni kwasababu zifuatazo , Moja ni baadhi ya watu kusema kuwa katika kampeni za uchaguzi Tido aliweza kutoa mchango mkubwa sana katika kutokuwa na upendeleo katika kutoa habari za uchaguzi na wengine kusema kuwa ndio kisa chake cha yeye leo serikali kusitisha mkataba wake.

Lakini ukweli ni kwamba katika kampeni ni wazi kila mpenda maendeleo alikilalamikia chombo cha habari cha TBC ambacho maana yoyote ile hakikupaswa kuegemea upande wowote ule katika kampeni lakini chombo hicho kilikuwa sambamba na chama tawala.
Sababu zilizopelekea vyama vya upinzani kulalamika sana katika utoaji wa habari za kampeni lakini kwanini leo watanzania hao hao wanashabikia kuwa Tido Mhando alikuwa hana upendeleo akiwa kama mkurugenzi wa TBC?

Hapa najiuliza maswali mengi sana ni muda mfupi tu umepita Watanzania wamashasahu mapema hivi hili linaonesha jinsi gani watanzania tulivyo wasahaulifu.Kwanini tunapenda kuita rangi nyeupe kuwa nyeusi? Ni nini hasa mnachosifia Tido na kuleta madai kuwa sababu za yeye kupendelea CHADEMA ndio kisa cha mkataba wake kusitishwa?

Mimi naamini Tido ni mchapa kazi lakini kwa kusema leo kuwa hakuwa na upendeleo katika kampeni ni Unafiki Mkubwa wa Watanzania.Tuacheni unafiki penye ukweli tuwe wakweli daima hayo ya unafiki ndio yanatufanya kila siku kubaki kulalamika uongozi mbaya na mambo mengine .Wana JF najua kila mmoja amelipokea hili kivyake ila mimi nasema Unafiki Mbaya tuacheni .
 

Forum statistics

Threads 1,237,001
Members 475,398
Posts 29,275,537