Watanzania kufurahia bifu la Marekani na Korea ya Kaskazini ni ufahari au ni kukengeuka kiakili?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Rejea tu Kichwa cha habari hapo juu na karibu katika utiririkaji wako.

Nawasilisha.
 
Ujinga tu, watu hata hawajui vita maanayake nini?

Kweli Mkuu na ukija huku Vijiweni kwetu utashangaa kwani utakuta Watu wanaielezea Marekani na Korea Kaskazini Kivita utadhani wao ni Wamarekani au Wakorea Kaskazini na wengine wako tayari kupoteza muda wao kuifuatilia hii bifu kuliko hata kufuatilia maendeleo ya Babu na Bibi zao huko Vijijini pamoja na Mbuzi zao zinazozaana huko na zimekosa malisho.

Waswahili ni Watu wa ajabu na Wapuuzi sana hakyanani!
 
Sio sawa.
Ila ni vizuri kwa watanzania wote wakawa na ufahamu wa vitu vinavyoendelea duniani.
Dunia sio kijiji tena, imekuwa familia hivyo chochote kinachotokea ndani ya familia ni vizuri wote tukawa na mirejesho.

Ila fafanua Kukengeuka kiakili unamaanisha nini mkuu. Maana ukiangalia Comments za watu wengi kwenye mitandao mingi ulimwenguni hayapishani sana na ushabiki huu wa bongo.
 
Kweli Mkuu na ukija huku Vijiweni kwetu utashangaa kwani utakuta Watu wanaielezea Marekani na Korea Kaskazini Kivita utadhani wao ni Wamarekani au Wakorea Kaskazini na wengine wako tayari kupoteza muda wao kuifuatilia hii bifu kuliko hata kufuatilia maendeleo ya Babu na Bibi zao huko Vijijini pamoja na Mbuzi zao zinazozaana huko na zimekosa malisho.

Waswahili ni Watu wa ajabu na Wapuuzi sana hakyanani!
Aaaah refa unaibeba yanga. Ila Kichukua anakuja.
 
Ujinga tu, watu hata hawajui vita maanayake nini?
Sasa ni vizuri ungeelimisha kwanza "vita ni nini"....halafu badala ya hapo ndo tupate kipimo kama ni ujinga au sio ujinga.

Binafsi naona kufurahia naona si vizuri.........ingawa kuna muda mambo haya hutokea ili dunia iendelee kuwepo katika mizani sawa (balanced).
 
Hivi Referee wa anayechezesha mechi ya Simba na Yanga akiwa uwanjani tayari kupuliza Kipyenga anaweza kuulizwa Yeye anashabikia Timu gani au anaona Timu gani itashinda?

Tatizo lako lako unajua kuchomoa maswali ili upime uwezo wa mtu.

Mimi binafi naona hayo mambo ya vita vyao tuwaachie wenyewe. Sisi tupambane na vita yeti ya maisha ya kitanzania, kwani adui yeti anaonyesha katukamia has a sisi tunaomkamia na maneno ya ukweli.
 
Cha ajabu wao huko hata hawatuzungumziagi na hawajui kuwa kuna nchi inaitwa Tanzania bali kuna "Nchi inaitwa Africa".

Ila kiukweli Kwa mtafutaji lazima aikubali North Korea, Nchi imewekewa vikwazo vya kila aina lakini bado ina jikongoja. Salute sana hawa jamaa!
 
Back
Top Bottom