Watanzania jiungeni na CCM la sivyo mtaendelea kupiga kelele zisizo na malengo

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,685
11,988
Nawashauri Watanzania hasa vijana mjiunge na ccm mfaidi keki ya nchi la sivyo keki ya nchi itakuwa inaliwa na wajanja wachache pamoja na wahamiaji wanaokuja kutafuta fursa nchini Tanzania

Vijana wengi wa kitanzania ni fuata mkumbo hawajui kuyatafakari mambo kwa kina
Wasichojua kuwa Tanzania ni nchi ya ki communist hiyo demokrasia ni geresha tu ili mabeberu yasiisumbue nchi yetu

Ila kikweli mfumo unaofanya kazi nchini Tanzania ni mfumo wa chama kimoja

Ndio maana hata palipohitajika kuanzisha siasa ya vyama vingi Mzee Nyerere alimuandaa rafiki yake wa siku nyingi mzee mtei namna ya kuunda chama cha siasa vile vile aliwaandaa majasusi kina marando na kina mbatia namna ya kuendesha siasa hata Caf ya maalim seif inabaraka za mwinyi

Kikubwa asilimia 97% ya vyama vya siasa nchini vimeanzia ndani ya ccm hata yule kijana wakigoma chama chake kina baraka za jk' bila jk asingeweza kusajili

Sasa basi wasichojua vijana wanagawanywa ili kundi la watu wachache waendelee kuitafuna nchi huku miaka ikienda mbele
Vijana acheni kujitoa ufahamu jiungeni na ccm mkapambane mpate nafasi ya kuongoza nchi

Kiufupi ccm haiwezi kutoka madarakani kutoka madarakani kwa ccm labda ibadili jina kama ilivyobadili kutoka TANU

Huu ni ukweli mchungu ambao vijana hawawezi kuikabili hata ukifuatilia siasa za uchina sio kwamba watu wote wanaridhika na mfumo huo ila kwa kuwa waasisi waliamua nchi iendeshwe hivyo Hakuna wa kubadilisha

Vijana mtaendelea kupewa matumaini hivyo mara Tundu lissu atashinda urais mara mbatia atashinda urais ili muendelee kubaki huko msiingie ccm wenzenu waendelee kula

Matokea yake wageni kama wahindi,waarabu,wasomali wanatumia udhaifu wetu wa fkra tofauti kujinufaisha ndani ya ccm na wanakuwa na ushawahishi ndani ya nchi Kuliko nyie wamatumbi ambao ni wazawa

Acheni ujinga jiungeni na ccm,msilalamike ccm kuna mafisadi wewe unajukumu la kwenda kupambana na mafisadi kama magufuli anavyoyashughulikia akiwa Ndani ya ccm

Kuna vijana wanajipa matumaini ccm itavunjika hizo ni ndoto za mchana kwa mfumo wa CCM wa kicomunist hiki chama kipo sana kwa karne moja ijayo

Nyie endeleeni kususa huku kundi fulani likifaidi nchi

Ila kama mnataka mabadiliko jiungeni na ccm myatafute mabadiliko
 
Leta porojo tuu za kujifurahisha, lakini game la Octoba 2020 ni Membe (CCM) na ??? (Upinzani).
Kama CCM baada ya hapo itakufa au ita pona shauri yenu mtajijua wenyewe.
 
Watu wameanza kugawana mbao halafu unasema vijana wa jiunge na CCM wafaidi keki ya taifa,labda kama keki yenyewe ndo mbao zenyewe za kufaidi utawapata wengi wa kugawana mbao pasu kwa pasu zingine CCM mpya na zingine CCM asili.
 
Unafurahisha mkuu mi nawaomba endeleeni kutafuna Pesa ya membe ili zipungue maana Huyo Mzee ameifilisi sana nchi
Leta porojo tuu za kujifurahisha, lakini game la Octoba 2020 ni Membe (CCM) na ??? (Upinzani).
Kama CCM baada ya hapo itakufa au ita pona shauri yenu mtajijua wenyewe.
 
Kama unadhani membe yuko mwenyewe. Kuna chenge( fisad hd.. na huyu alishajisifu kuwa hakuna wa kumfunga. Na kweli serikal haijawahi mgusa).
Kuna rostam.. na wengine.. na wote ndani ya ccm.
Lakin ccm imewakaushia
Unafurahisha mkuu mi nawaomba endeleeni kutafuna Pesa ya membe ili zipungue maana Huyo Mzee ameifilisi sana nchi
 
Ni jukumu letu kupambana nao hao tukiwa nje ya ccm hatutapata kitu
Kama unadhani membe yuko mwenyewe. Kuna chenge( fisad hd.. na huyu alishajisifu kuwa hakuna wa kumfunga. Na kweli serikal haijawahi mgusa).
Kuna rostam.. na wengine.. na wote ndani ya ccm.
Lakin ccm imewakaushia
 
Write your reply...maisha ya watanzania hayawezi kuboreshwa kwa kuvalishwa nguo za kijani nchi nzima. mkijiunga nyie wanafiki wachache, mnatosha!
 
Unaongelea CCM ipi?

Kinana na Makamba mpk wameshakua makatibu wakuu wa CCM lkn mpk leo hii wao wenyewe wameshindwa kuielewa CCM inataka nini.

Utakuja kua wewe wa buku 7 FC.
 
Mbona huko CCM ndio kuna kelele nyingi zaidi zisizo na malengo? Jitakaseni kwanza kisha mualike watu kujiunga nanyi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom