gwamaka aswile
Senior Member
- Mar 26, 2015
- 186
- 106
Kufuatia ndugu John Pombe Magufuli kuchaguliwa kwa kura nyingi na CCM kuwa mgombea urais kupitia chama hicho, napenda kuwaasa Watanzania bila kujali itikadi zao za vyama kumchagua katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu kwani ndiye pekee atakayeliongoza taifa hili kwa kufuata misingi ya utawala bora na kuliletea taifa letu maendeleo kwani ana sifa za kuwa rais wetu. Natoa rai hiyo kwa sababu Magufuli ni mchapakazi mzuri hakuna Mtanzania ambaye atajaribu kujitokeza na kupinga kauli yangu. Shime Watanzania, tumchague Magufuli na kuachana na poropoganda zinazopigwa na watu wachache ambao siyo wa wazalendo wa nchi yetu ambao wanadai CCM haijafanya mazuri wakati wao wamesoma hadi kufika vyuo vikuuu kwa sera nzuri za chama hicho.