Pundadlimia07,
Mkuu wangu hata mimi ningemchagua anayetaka kujenga uwanja.. Huu ni mchezo wa mpira, ujenzi wa kiwanja ndio unaweza kuongeza pato la club na biashara nzima huanzia hapo.. Utathibiti fedha vipi, ikiwa club yenyewe haiwezi hata kuwa na kipato zaidi ya mgao wa shirikisho la michezo. hiyo fedha ya kuthibiti inatoka wapi?.. michango ya wanachama! si kutiana umaskini mkuu wangu.
Mimi nakubaliana na hoja hii ya kutopenda kuambiwa ukweli lakini siku zote huwezi kumshirikisha mtu kwa ufisadi kwa sababu yeye kalaani Ufisadi. tatizo la watanzania hawataki kuambiwa ukweli linatangulia na hoja ya kwanza. Tumalize kwanza kuwasafisha mafisadi waliopo kisha kesi ya Sitta itafuata kama naye ni fisadi.. Kilichotokea hapa ni kwamba Sitta analaaniwa kwa sababu he is against Mafisadi. Tunajua fika kwamba Mwakyembe na mama Kilango wote hawa wametajwa kwa mabaya yao toka wasimame dhidi ya Mafisadi.
Na ukiangalia kwa undani, report ya mafisadi Mwakyembe hakuandaa peke yake.likuwa kamati nzima leo kila neno baya anazungumzwa Mwakyembe hatujawasikia tena wajumbe wengine wakizungumzwa wala wao kufungua vinywa vyao. Ndio hadithi hizo, Mengi fisadi, Mbowe fisadi, Dr.Slaa fisadi, Zitto fisadi lakini husikii wakisema viopngozi wengine ngazi hizo hizo toka vyama vingine kwa sababu tu wamekaa kimya kuhusiana na mafisadi!
Sasa tujiulize iweje kila anayesimama against mafisadi, kesho yake tu ndio hadithi kubwa magazetini, tutaletewa Ufisadi wao hadi maisha wanayoishi na wake au waume zao...tena basi wakati mwingine huo ukweli wenyewe hauingii hata akilini..
Sitta ni mtu powerful ktk serikali yetu, ni mtu wa tatu baada ya rais..yupo juu ya PM na mawaziri wote kikatiba kwani anaweza kushika kiti cha IKULU inapobidi.. Hivyo kukodishiwa nyumba ya dollar 7,000 kwa mwezi wakati kuna nyumba za kawaida zinapangishwa kwa dollar 3000 kwa mwezi wala sioni kitu cha ajabu sana..zaidi ya kushangaa matumizi makubwa ya serikali yetu kwa ujumla wake. I mean ni kiasi gani serikali inalipa viongozi wetu wote, tazama ukubwa wake, miradi isokuwa na maslahi kabisa toka enzi za Mkapa..... bila shaka wanalipwa kuliko viongozi wa nchi tajiri duniani..
Tusishangae hilo na kuiita serikali nzima ya kifisadi bali tunachagua baadhi ya watu wanaodai kukomesha ufisadi unaoitambulika wazi..Hivi ni kiasi gani cha fedha kinatugharimu ktk kukodisha nyumba wakati serikali ilikuwa na nyumba zake! Mkapa kauza nyumba zote watu wakamshangilia sana na wanasema hana makosa, leo Sitta kakodishiwa nyumba kutokana na makosa ya Mkapa inaonekana ni ufisadi.. how about wale walionunua nyumba za thamani ya mabillioni kwa dollar 20,000, hawa sio mafisadi na tuwataje wote basi.. ndio ukweli unavyoweza kukubalika kwani hata mnunuzi anaweza kuwa fisadi hata kama ndio bei iliyotolewa na serikali...