Tatizo kubwa sana sasa kwenye nchi yetu sio wanasiasa bali ni Watanzania wote kwa ujumla kama nchi. Watanzania tumekuwa nchi kama mpya vile wengi wetu ni wavivu wa kufikiri, washabiki wa mambo yasiyo na tija kwa nchi na hatari na hatujui tunataka nini.
Kwenye nchi nyingi kuna misimamo ya wananchi mfano DRC wanataka uchaguzi huru, China wananchi hawajali siasa wao ni uchumi imara, US demokrasia ya watu na haki. Je sisi tunasiamama kwa lipi ambalo tunawaonyesha wanasiasa au mtu yeyote kwamba hapa tuna umoja. Je tunasimama kwa katiba ya nchi? Wakati tunaona katiba ina kiukwa waziwazi na hatusemi chochote, Je tunasimama kwenye demokrasia? Mbona tunaona demokrasia inakiukwa waziwazi bila kufanya lolote, Je tunasimama kwa uchumi? Mbona wafanyabiashara wana nyanyaswa bila kusema lolote mfano kodi, maduka kufugwa na kulipishwa laki saba kabla hata ya kipato ukifungua duka. Je tunajali Utanzania na uraia? Mbona kuna wenzetu kisiasa tu wanaambiwa sio raia na tumenyamaza wengi. Je ni usalama? Mbona wabunge wanapigwa risasi, wafanyabiashara wanatekwa bila kusimama pamoja.
Tatizo letu tunategemea wanasiasa watuletee mabadiliko wakati wenyewe ndiyo wameleta hayo matatizo. Sasa Watanzania kwa serikali tumekuwa kama houseboy mvivu ambaye anapelekwa tu lakini naye hawazi kufanya maamuzi. Tumekuwa na uzuba wa hali ya juu. Tusikokuwa waangalifu itachukuwa miaka mengi kurudisha nchi yetu pazuri. Hatuwezi kulalamikia wanasiasa ambao wanafuata wananchi na wananchi hawaeleweki misimamo yao