WaTanzania Hakuna Aliyeturoga: Tumekosa Maarifa Kwa Kuweka Kila Kitu Kiongozwe za Siasa

EWGM's

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,523
2,000
Huu mchezo wala hautaki hasira na pia napenda kuwahakikishieni hakuna aliyeturoga lazima tukubali waTanzania tumekosa maarifa na siku tutakapo weka akili zetu sawa ndiyo tutajua kuwa wanasiasa wanatuchezea akili zetu.

Mwenye kusoma na asome na mwenye kuelewa aelwe. Soma kwa ufasaha na kwa umakini sana hii barua ndefu yenye maelezo mengi halafu tazama chini yake word to word transcript ya Prof. John L. Thornton.
"I have come here in order to help resolve the problem and I assure the President that we are interested in sitting down and reaching a resolution which is a win win (A win for Tanzania and a win for Barrick and our Subsidiary company, ACACIA)

After having these extensive conversations I feel very optimistic that we will reach a resolution which is a win win for all parties and we will be sitting down soon with a team designated by the President and our own team to go through the detail of that and I feel very good about the progress today.
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
11,981
2,000
so tunapigwa changa la macho! is word prove that or action..?
 
Lizarazu

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
6,151
2,000
Juzi kapokea ripoti na kukubali mapendekezo yote ya kamati. Mojawapo ya pendekezo ni kuwachukulia hatua na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola wote waliohusika.

Leo kakutana Ikulu na mmoja wa watuhumiwa na kukubali kuyazungumza.

Aliyeturoga sijui ni nani?
Kwenye blue, unataka kumaanisha kwamba huyo professor nani nani sijui kutoka Canada leo hii pale pale ikulu angepigwa pingu na kupelekwa kizuizini ama!?
 
john agrey

JF-Expert Member
Jan 24, 2015
1,254
2,000
Kwenye blue, unataka kumaanisha kwamba huyo professor nani nani sijui kutoka Canada leo hii pale pale ikulu angepigwa pingu na kupelekwa kizuizini ama!?
Ndio maana yake mwizi ni mwizi tu awe mzungu awe mwafrika awe bashite awe professor ni mwiziiii tu he deserve same treatment as the young Tanzanians who are killed on the street sometimes with wrong accusations of theft cases
 
kg1

Senior Member
May 27, 2017
152
225
Huu mchezo wala hautaki hasira na pia napenda kuwahakikishieni hakuna aliyeturoga lazima tukubali waTanzania tumekosa maarifa na siku tutakapo weka akili zetu sawa ndiyo tutajua kuwa wanasiasa wanatuchezea akili zetu.

Mwenye kusoma na asome na mwenye kuelewa aelwe. Soma kwa ufasaha na kwa umakini sana hii barua ndefu yenye maelezo mengi halafu tazama chini yake word to word transcript ya Prof. John L. Thornton.
"I have come here in order to help resolve the problem and I assure the President that we are interested in sitting down and reaching a resolution which is a win win (A win for Tanzania and a win for Barrick and our Subsidiary company, ACACIA)

After having these extensive conversations I feel very optimistic that we will reach a resolution which is a win win for all parties and we will be sitting down soon with a team designated by the President and our own team to go through the detail of that and I feel very good about the progress today.
Hizo ni kelele tu, mbona hayo ni ya zamani?
 
Lizarazu

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
6,151
2,000
Ndio maana yake mwizi ni mwizi tu awe mzungu awe mwafrika awe bashite awe professor ni mwiziiii tu he deserve same treatment as the young Tanzanians who are killed on the street sometimes with wrong accusations of theft cases
Sasa kwanini hakumkamata na kumtia kizuizini pale pale wakati tayari ushaidi upo mezani!?

Sheria inasema muovu yeyote wa jinai mara tu inapothibitika anastahili kukamatwa mahali popote anapopatikana, sasa kama kweli hao Barrick corporation ni wenye hatia, ina maana kwamba huyo mwenye kiti wao aliokuja Leo ikulu ndio mastermind wa kila kitu yaani kwa maana nyingine yeye ndio jambazi kuu. Sasa nashangaa leo amekuja na kupokelewa kama mfalme ndani ya nyumba kuu wakati tayari tumeshatangaza vita na yeye pamoja genge lake.

Hizo stori za kwamba watalipa hayo matrilioni ni sawa na kumbembeleza mtoto mdogo uliyetoka kumchapa hivi punde kwa kumuhaidi kwamba utamnunulia peremende wakati huo ukiwa unajua kabisa atasahau.

Hilo suala la kuwatia nguvuni hao jamaa mnaweza kulifanya kupitia contract readjustment na wala sio kingine.
 
EWGM's

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,523
2,000
Ndio mkuu nimeyapima vizuri nimeona yanafaa na mwanzo mzuri. Prof john ilikua ni lazima aongee vile kwakua yeye ndio mwenye uhitaji na sisi.

Kuna kitu pale lazima uelewe, niliwahi kusoma sehemu wasio na maarifa huwa wana-react kwenye mambo/jambo lakini wenye maarifa wana-respond. Mtu anayerespond hutengeneza mangira ya kujipanga. Ile kauli ya Prof John ni kupoza hali ya hewa ili shughuri zianze kuendelea kama kawaida huku wao wakijipanga kurespond kimkakati.

Sababu kauli aliyotoa JPM ni tofauti sana na Prof JT pia kuna sehemu alitaka kumlisha maneno lakini akatikisha kichwa tu, na wakati Prof JT anaongea JPM alionyesha kuna kitu hakupendezwa nacho cha kumfuata waziri wa sheria.

Lakini siku zote muda ni mwalimu
 
utali

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
611
500
Ndio mkuu nimeyapima vizuri nimeona yanafaa na mwanzo mzuri. Prof john ilikua ni lazima aongee vile kwakua yeye ndio mwenye uhitaji na sisi.
Tatizo letu kubwa pia ni uelewa. Ukifuatilia kwa umakini hili suala la madini na mikataba utaona kwamba matatizo yote haya kwa kiasi kikubwa yametokana na makosa yetu wenyewe. Kuanzia sheria zetu, uelewa wa watia sahihi mikataba, ubinafsi hadi usimamizi.
Sasa kama sisi wenyewe tuliruhusu kuibiwa, kwanini hao jamaa wasituibie. Mtu ana declare 20tons za mchanga kwenye container halafu sisi hata kukagua ili kujiridhisha kuwa ni 20tons halisi hatufanyi hivyo, kwanini jamaa wasiongeze japo 4tons ktk kila container??
Mimi sioni ajabu kwa huyo Prof wa Barick kuja na kuzungumza ili twende sawa maana makosa ni ya kwetu wenyewe na kwa kuwa tumetambua hilo wao wako tayari kukaa mezani ili tuzungumze na sasa kiubinadamu na kiimani na hata kujenga heshima ndio maana wako tayari kutulipa hicho tulichostahili kupata.
Hata hivyo uamuzi wa mwisho wa kuendelea kufanya nao biznes ama la ni wetu lakini bado tunahitaji kuyachimba hayo madini na kuyauza regardless of who will be doing biznes with.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom