Gambamala
JF-Expert Member
- May 13, 2014
- 1,045
- 766
Watanzania wenzangu, nadhani wakati umefika sasa Watanzania wote tuungane, tuwaulize Tanesco nini kinawasibu. Kama kuna kero kubwa nchi hii, mojawapo ni upatikanaji wa umeme wa kudumu. Kwa sasa kupata umeme masaa 24 kwa siku tano imekuwa jambo la nadra. Haijarishi ni masika au kiangazi. Binafsi, na wananchi wengine ambao tumekuwa tukitegemea umeme tumerudi nyuma kimaendeleo kwa ukosefu wa umeme. Mwezi wa Novemba 2015 tuliambiwa mabomba ya gesi yanajazwa ili tupate umeme wa gesi, lakini hadi leo hayo mabomba hayajai. Mimi naomba Tanesco waitishe harambee ili Watanzania tutoe michango yetu ili kuondokana na hii kero. This is too much, mtu unaamka asubuhi huna uhakika kama kazi yako utaitimiza kutokana na ukatikaji wa umeme.