Watanzania bado tunakumbuka uharifu huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania bado tunakumbuka uharifu huu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakende, Sep 17, 2012.

 1. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ungawa siku zimepita lakini ni vuzuri kuendelea kukumbushana, najua kuwa mengi mabaya yamefanyika lakini jambo hili ni zito ingawa watu wengi uchukulia rahisi.

  Katika serikali ya hawamu ya tatu (Mkapa) viongozi wa serikali na baadhi ya waajiriwa wa Serikali walihamua kugawana nyumba za umma kwa bei ya kutupa bila kujari nyumba ni potential kwa kiasi gani. Tumeshuhudia ufisadi wa kututisha lakini kusema ukweli huu ndiyo ulikuwa hatari zaidi kuwahi kutokea katika nchi yetu.

  Watanzania uchukulia rahisi jambo hili, lakini ukitaka kujua ni zito kiasi gani ebu jaribu kutathimini thamani ya nyumba na ujaribu kufikiria nyumba zote za serikali nchi nzima ndipo utakapotambua kuwa ni trioni ngapi za pesa zilipotea ndani ya muda mfupi.

  Nyumba ziliuzwa bila kufuata sheria za uuzaji wa mali za umma, si watanzania wote walipewa nafasi ya kununua nyumba hizo maana hata tenda hazikutangazwa. Walionufaika wakati huo ni wale wenye ubavu, yaani viongozi wa juu wa nchi pamoja na wakuu wa idara. Maana hata mimi nilishuhudia OCD akiwa amenunua nyumba ambayo inaangaliana na kituo cha polisi, sijui siku hizi kama bado anaishi hapo.

  Baada ya miezi sita, tulishuhudia serikali hiyohiyo ikiangaika kuwapangia hotel viongozi baada ya kukosa makazi. Hadi sasa bado serikali inawalipia kodi wafanyakazi wa juu katika nyumba za watu binafsi

  Mimi naamini iko siku, hizi nyumba zitarudi kwa njia yoyote ile, hao wanao ishi humo wajue wapo kwa muda tu, ni kama wapangaji wa muda mrefu wakisubuiri CCM ing'oke
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  "Uharifu" ndio nini?
   
Loading...