Pia ukiangalia kwa ukaribu hao watu hawana the same mood.Nimeangalia picha nyingi za CCM zote hadira ni ile ile,wingi wa watu ni ule ule,jamani tunaenda mikoani kuna mikoa au wilaya watu siyo wengi kiasi hicho.
Nimewahi kuiona ya Samia Suluhu akiwa jimbo la Mbowe kwenye TV na gazetini haina tofauti na hiyo iliyoletwa humu.Jamani haiwezekani.
Tuseme ukweli,na msema ukweli mpenzi wa Mungu.Tusiwe tunajidanganya kila wakati.
Bado nasema tusijidanganye na siyo kwa CCM tu hata upinzani,niliwahi kulieleza hilo.TUSIJIDANGANYE,siyo kila mahali utapata watu wale wale,wenye nguo na rangi zile zile,duh.
Toka harakati za kugombea urais kwenye nchi hii yeye pekee yake ndio kaja na style hii ya kugeuza jukwaa kuwa SEHEMU YA KUFANYIA MAZOEZI kama si kukosa sera ni nini?wapi kwingine yalifanyika kama hayo,haelewi kuwa kuna nchi alichaguliwa mgombea anasukumwa kwenye wheelchair.sera zinazokosa nguvu ya utekelezaji ni sawa na wimbo wa taifa tu.