Watano wakamatwa na mihadarati Morogoro

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata watuhumiwa watano kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya ikiwemo bangi kilo mia moja, mirungi kilo sitini, heroine kete tatu na vifungashio vya dawa hizo katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro, ikiwa ni jitihada za kuendeleza vita dhidi ya matumizi na uuzaji wa dawa hizo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wamekamatwakatika maeneo tofauti ya mkoa wa Morogoro ikiwemo wilaya za Mvomero, Morogoro manispaana Kilombero,wakiwemo watuhumiwa waliokuwa wakisafirisha dawa hizo kwa magari ya abiria, basi la BM Coach huko Mkindo Turiani, na gari ndogo aina ya Hiace maeneo ya Kihonda, pamoja na pikipiki maarufu kama boda boda.

Baadhi ya watuhumiwa waliohojiwa kuhusiana nadawa hizo, wamekuwa na majibu tofauti, wengi wakidai kutumwa na watu mizigo hiyo ikiwemo mirungi na bangi, ambapo aliyekuwa amebeba debe nne za bangi kwa kuficha ndizi mbichi juu ya kiroba kilichokuwa na mzigo huo akidai alitumwa na mtu bila kujua mzigo huo kama ni bangi, ambapo polisi wameomba ushirikiano zaidi kuwabaini na kufichua matukio ya dawa za kulevya na watuhumiwa wake.

 
Back
Top Bottom