Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 811
- 1,870
Helikopta ya kampuni ya uokoaji Kilimediair Aviation imepata ajali katika Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania na kusababisha vifo vya watu watano, wakiwemo raia wa kigeni wawili, rubani na daktari.
Ajali hiyo imetokea Jumatano ya Desemba 24 , katika eneo lililopo kati ya kilele cha Kibo na Barafu Camp, moja ya njia zinazotumiwa sana na watalii wapandaji wa mlima huo mrefu barani Afrika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, akieleza kuwa helikopta hiyo ilikuwa katika zoezi la kuwachukua wagonjwa waliokuwa wamepandishwa mlimani na kampuni ya utalii ya Boby Camping.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, waliopoteza maisha ni wageni, muongoza utalii mmoja, rubani wa helikopta pamoja na daktari, aliyekuwa sehemu ya timu ya uokoaji.
Chanzo Na Bbc Swahili