Watano mbaroni Dar kwa kupora gari

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KIKOSI Maalumu cha Kupambana na Wizi wa Magari, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kimewakamata watuhumiwa watano akiwemo mfanyabiashara Ndama Shabani (38) maarufu kama Ndama Mtoto wa ng’ombe kwa tuhuma za kupora gari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Naibu Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova alisema gari hilo ni aina ya Hino yenye namba ya chesisi FDIJKD 11185, liliporwa Tunduma mkoani Mbeya.

Alidai kuwa Ndama ambaye pia ni mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam, alishirikiana na wenzake, Silvester Mashindila (45), Richard Marimi (46), mkazi wa Mwananyamala kwa Kopa, Peter Goyayi (30) maarufu kama Makoye, mkazi wa Mwananyamala, Charles Mwita (43), Mkazi wa Kinondoni.

Kwa mujibu kamanda huyo, baada ya watuhumiwa hao kupora gari hilo huko Mbeya, walikimbilia mafichoni Dar es Salaam nyumbani kwa Ndama na kutokana na juhudi za Polisi walitiwa mbaroni.

Gari hilo linadaiwa lilikuwa limesheheni mali na bidhaa mbalimbali vikiwemo vitanda vinne, magodoro, majokofu, makochi na majiko ya umeme.

Kamanda Kova alisema mali zote zimekamatwa na Polisi pamoja na gari hilo na kesi ya wizi huo imefunguliwa mkoani Mbeya.

Katika hatua nyingine, Kova alitoa mwito kwa vijana ambao wamemaliza elimu ya msingi au sekondari na kushindwa kuendelea na masomo, kujiunga kwenye mchezo wa ngumi za kulipwa ili wapate ajira badala ya kujiingiza katika matukio ya uhalifu.

“Natoa rai kwa vijana waliokosa ajira kujiunga na ngumi za kulipwa na michezo mingine badala ya kutumia nguvu zao katika uporaji au uhalifu wa aina yoyote maana wataishia pabaya,” alisema.

Kova alitoa rai hiyo wakati akimpongeza Karama Nyalawila aliyepata ubingwa wa dunia katika masumbwi na kuahidi kumsaidi katika kugharimia mazoezi yote atakayotakiwa kufanya.
 
Back
Top Bottom