Mkuu kuhusu timu yake ya Taifa hakuwa na namba ya kudumu labda mwaka juzi kurudi nyuma, kawaulize Angola wanajua alichokifanya leo kwenye mechi iliyochezwa kwenye ardhi yao wakati walijiaminisha kuwa wametoka na ushindi, huku kiungo bora kabisa wa Yanga na timu ya Taifa ya Rwanda kashindwa kuisaidia timu yake.Uliona wapi mchezaji asiyekuwa hata na namba ya kudumu kwenye kikosi chake cha Taifa akauzwa kwa bei hiyo?
Mkuu kuhusu timu yake ya Taifa hakuwa na namba ya kudumu labda mwaka juzi kurudi nyuma, kawaulize Angola wanajua alichokifanya leo kwenye mechi iliyochezwa kwenye ardhi yao wakati walijiaminisha kuwa wametoka na ushindi, huku kiungo bora kabisa wa Yanga na timu ya Taifa ya Rwanda kashindwa kuisaidia timu yake.
Hiyo ya kukosa magoli ya wazi hata mimi nimeisikia sina hakika kama ni mengi ila ya kuomba samahani sijasikia, lakini kwa nini kocha amkasikirikie na waganda wamlaumu yeye wakati kacheza dakika 32 tu na kuna washambuliaji wengine wamecheza dakika 90 kwa nini wasiwalaumu hao wengine na kama wengine walikuwa hawapati nafasi maana yake yeye ni bora kaingia na kucreate nafasi zote hizo ingawa bahati haikuwa upande wake, mkuu kubalini tu dogo kwa sasa ni jembe, kwa nchi zote za Afrika mashariki ndo mchezaji pekee aliyetikisa nyavu ktk mechi za mwisho wa wiki, tukifanikiwa kuziba pengo la Mafisango natamani tumpate kiungo mwingine kama Niyonzima au Niyonzima mwenyewe atuchezee namba nane, tukifanikiwa hiyo safu ya mbele itatisha.Mkuu(Masuke) kuna habari nimezipata sijui unaweza ukanithibitishia?
Ni kwamba nasikia "Jiwe letu la Almasi" Okwi pamoja na kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Angola juzi lkn alishindwa kuitetea thamani yake ya Billion 2...,alikosa magoli ya wazi takribani 9 hivi hali iliyomchukiza sana Kocha wake na hata Waganda wote waliokuwa wanaufatilia mtanange ule kiasi kwamba amelazimika kuwaomba radhi waganda wote kwa kuonyesha kiwango cha chini katika mechi ile,unaweza kunithibitishia haya ndugu yangu,samahani lkn!
yule m'popo wa El Merreikh ya sudan alilipiwa kitu cha 2.5 B(anaitwa Worgu kama sikosei).kaja hapa kagame iliyopita anakaanga bisi uwanjani.sioni kama haiwezekani mkuu na zaidi sioni kwanini ikutoe povu namna hii!
Si mmeshamchukua Yondani kwa nini mnatufuatafuata, tuacheni na Okwi wetu na bilioni zake mbili.Somebody anijuze jamani,
Hivi hawa viongozi wa Simba huwa wanatumia kilevi gani,Chimpumu,Pingu,Biwa ama Chang'aa...mana'ke jana Mheshimiwa Aden (Maha)Rage kaja na bei mpya ya Okwi,nasikia sasa wanamuuza kwa Mil 950 na maelewano yapo,kutoka Million 2000 iliyokuwa imetangazwa na Msemaji wa Club hadi Mill 950 pungufu unaongea,....pamoja na baadhi ya wadau wa Simba hapa JF kunipinga waki'insist kuwa ile ndo thamani ya Okwi lkn nimefarijika kuona Mwenyekiti wa team baada ya kupitia hii thread yangu na yeye am'realise kuwa kuna mantiki katika hoja yangu hii,sasa naomba kumwambia Bwana Ismael Aden (Maha)Rage (najua huwa anapitia humu) kuwa bado Mill 950 ni nyingi kwa mchezaji wa kiwango cha Okwi,kama anania ya kumsaidia mchezaji husika na team kwa ujumla amweke sokoni kwa bei inayoendana na kiwango chake na a'set(katika makubaliano ya kumuuza) mipango inayoweza kuinufaisha team kwa kadri Mchezaji atakapokuwa anapata maendeleo mathalani kuuzwa katika Club kubwa,hivyo ndivyo viongozi makini wanavyofanya kazi aachane na mawazo yanayotolewa na kina Masuke,Ngarna,Ngotimbezi,Crashwise na wengineo wanao'tapika humu ndani.