Watangazaji wetu na weledi wao!

Watangazaji wetu na weledi wao!

Jana nilikuwa natazama taarifa ya habari saa moja usiku kupitia kituo cha luninga cha Channel Ten, nilipata ukakasi baada ya kumsikiliza mtangazaji wa habari za kimataifa akipata taabu kutamka mji wa Munich

Hili alilitaja kimakosa kama mara nne mpaka nikajiuliza ina maana hajawahi hata kulisikia neno hili kabla, ili ajisahihishe?

Leo ninasikiliza Radio Free Africa kipindi cha Watanzania Tuzungumze magazeti, mtangazaji ameanza na gazeti la Nipashe anatamka chama cha wanasheria Tanganyika kama TLC badala ya TLS. Amerudia tena kutamka TLC akipitia gazeti la Mtanzania.

MY TAKE:
Huwezi kujua kutamka maneno yote hasa yale ya lugha za kigeni kama kijerumani na kifaransa, lakini kama mtangazaji ni vizuri ukajiridhisha kama sehemu ya maandalizi ya kipindi jinsi ya kutamka maneno yaliyopo kwenye kipindi chako.

Tuweze kuwa mazoea ya kuwa na uwanja mpana wa ufahamu wa mambo yanayotuzunguka katika taaluma zetu, mfano mtangazaji wa taarifa za habari ni vema akawa mfuatiliaji wa habari mbalimbali zinazotangazwa na vyombo vingine hasa vya kimataifa badala ya kujikita kuchonga sauti peke yake.

The content is what matters the most.
Nenda WAPO REDIO utaishiwa nguvu, kutana na fadha Rupia hata jina lake husahau!
 
Msikilize Masanja Mkandamizaji WAPO REDIO: Enzi za Mwarimu saa hizi mmekwisha amka mnasikiriza habari mbarimbari sasa wewe umejifunika shuka amka usikirize WAPO REDIO.
 
Wachambuzi wengi wame muiga Dr Liki ila hawajui jamaa ana exposure sasa wao ili waonekane wabobezi basi utakuta wana chomeka na english matokeo yake ni kituko. Ata sijui ni redio gani ila mara nyingi nasikiaga nikiwa saloon nanyoa, hao wa EATV wanakuaga watatu aisee huwaga ni aibu. Wachambuzi tumieni kiswahili mwanzo mwisho, mnazingua sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa nakugeuzia kibao wewe mwenyewe. Hizo "huwaga" ndo Kiswahili cha wapi? Hakuna -ga ni makosa makubwa. Badilisha Kiswahili cjako. Pamoja tunaweza!
 
Nasikiaga
Wanakuaga

Haya ni makosa katika kiswahili.

Hahaa... ata wewe umefanya makosa ya kiuandishi pia! Mimi siyo mwandishi wa habari na hapa sipo darasani, ungejua historia yangu ungenipa hongera kwa kuandika hivi, kwa kifupi Kiswahili ni lugha yangu ya tatu kujifunza.

Hahaha!
Umenikamata hiyo 'typing error' lol!
Loh! Kumbe si m-tz. Kama hivyo hamna noma! Tupo pamoja mzeya.
 
Wana Matatizo sana ya kutokuwa watafiti na wachunguzi wa mambo yanaynhusu taaluma yao. Kituko Kingine ni utamkaji wa mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels wanautamka isivyo. Hata Dar Es Salaam Kuna baadhi ya watangazazaji wanaitamka kwa ukakasi sana. Kukosa weledi kupo pia kwenye taaluma zingine nyeti kama ualimu. Unakuta Mwalimu anatia aibu kwenye mambo ya ufahamu kuhusu fani yake hajui mambo mengi yaliyopo yahusuyo taaluma yake. Wanataaluma Wanapaswa Kuwa Wadadisi wa mambo mengi yahusuyo fani zao (well informed ).
Ukipanda upupu utvuna huohuo!
 
Hivi ukisema (ndo) ni kiunganishi sahihi au ni neno rasmi?
Nami nimekugeuzia kibao

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha hapo nakubali chief. Nimefanya makosa. A learned man hukubali kukosolewa. Binafsi, huwa ninajitahidi kukiboresha ili kuhakikisha Kiswahili changu kinakua kizuri. Nashukuru umwenionywsha hilo. Mambo ya kuchapa kwa haraka nayo ni chanzo chief. Kudos!
 
Clouds kuna mtangazaji amekuwa akilitumia neno "Aghalabu" kumaanisha "mara chache" badala ya neno "nadra". Lakini kuna huu ugonjwa wa kuweka herufi "r" mahala pa "l", sasa kuna mmoja alitamka "malazi" akimaanisha "maradhi".

Kibaya zaidi kuna ugonjwa mwingine ambao huu hauko kwa watangazaji tu bali umetapakaa kwa sehemu kubwa ya Watanzania na ambao nadhani tumeuiga kutoka Kenya wakati wa kujitambulisha utasikia mtu anasema "kwa majina naitwa....."; mimi sikumbuki kufundishwa hivyo katika kiswahili au kiingereza bali tulifunzwa "Jina langu ni (unayataja kama ni mawili, matau au zaidi"
 
ndiyo siyo ndio
Mkuu ndio na ndiyo yote ni maneno sahihi. Ndiyo huonyesha wingi, na, ndio ni umoja. Pia ufahamu ndiyo ni kukubali. Unapoandika sentensi na kutumia kama kiunganishi unaandika ndio na siyo neno NDIYO.

Mimi si mtaalam wa lugha. Nilijifunza kutoka kwa wataalam wa lugha matumizi ya maneno NDIO na NDIYO.
 
Walikupotosha, neno ni hilo hilo moja to la "ndiyo" ila muktadha wa matumizi yake ndyo unaoongoza namna ya kulitamka ili litoe maana inayokidhi muktadha husika. Nikupe mfano mwingine wa neno moja ambalo linaweza kumaanisha mambo mawili tofauti, neno hilo ni "barabara", kuna wakati linaweza kumaanisha njia na wakati mwingine kumaanisha sahihi/sawa/vizuri/haswa:
Barabara hii inaelekea.....;
Mambo yalikuwa barabara kabisa
 
Tukisha kariri na kufaulu mitiani...vyeti mkononi hakuna anayeangaika kujisomea na kujitafutia maarifa binafsi...vitabu tunatupa huko...angalau saaa tuna smart phones tunasoma angalau insta na facebook
 
Mkuu ndio na ndiyo yote ni maneno sahihi. Ndiyo huonyesha wingi, na, ndio ni umoja. Pia ufahamu ndiyo ni kukubali. Unapoandika sentensi na kutumia kama kiunganishi unaandika ndio na siyo neno NDIYO.

Mimi si mtaalam wa lugha. Nilijifunza kutoka kwa wataalam wa lugha matumizi ya maneno NDIO na NDIYO.
Aiseee, ulidanganywa mkuu. 'Ndio' ni umoja?
 
Back
Top Bottom