Bado narudia,sijaona kosa kubwa la mtangazaji wa kiswahili,nilichogundua tunataka mswahili atamke kwa lafudhi ya nchi husika,hilo haliwezekani kwa sababu hata mzungu (kulingana na taifa lake)hawezi tamka maneno ya kiswahili kwa lafudhi ya kiswahili lazima atagongagonga lafudhi,ndio maana kuna mataifa j wanaita h,eg mtangazaji mmoja aliyekuwa redio one alikuwa anaitwa josef ndamalya,kwenye taarifa ya habari anajitambulisha kama josef ndamalya,,kwenye mipasho utasikia anajiita hozee ndamalya
Boss nimegundua watu wana uelewa mdogo sana. Kuna mpumbavu mwingine eti kafungua thread kujibu nilichoandika.Unafahamu kwamba hata hao wazungu wa Uingereza au kwingine wakitaka kutamka jina kikamilifu huwa wanauliza hata ubalozi wa nchi husika?
Hivyo majina ya kichna, kikorea au mengine yakiwa magumu kutamka basi wenzio huomba masaada wa ubalozi husika na kujifunza kutamka hilo jina.
Hili ni jambo la kawaida kabisa kufanywa na watu wenye uelewa.
Halafu watangazaji wa redio khasa wa mpira si vibaya wakawa wanajifunza haya majina kwani huleta burudani pia wakisikika kuyatamka, wanaonekana wanafahamu na wana uelewa na hata mzungu akisikia atatamani kusikiliza hivyohivyo.
Kutamka jina hakuendani kabisa na mambo ya lafudhi unayoongolea.
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
Boss nimegundua watu wana uelewa mdogo sana. Kuna mpumbavu mwingine eti kafungua thread kujibu nilichoandika.
Bado narudia,sijaona kosa kubwa la mtangazaji wa kiswahili,nilichogundua tunataka mswahili atamke kwa lafudhi ya nchi husika,hilo haliwezekani kwa sababu hata mzungu (kulingana na taifa lake)hawezi tamka maneno ya kiswahili kwa lafudhi ya kiswahili lazima atagongagonga lafudhi,ndio maana kuna mataifa j wanaita h,eg mtangazaji mmoja aliyekuwa redio one alikuwa anaitwa josef ndamalya,kwenye taarifa ya habari anajitambulisha kama josef ndamalya,,kwenye mipasho utasikia anajiita hozee ndamalya
Mkuu umeelezea umuhimu wa nilichoandika kiufasaha zaidi.Zipo "tools" au zana na njia kadha wa kadha za kujifunza hivyo hii mada yako umeleta wakati sahihi na mahala sahihi maana wengine hata Kiswahili tu ni shida.
Hata kama umesoma au unafanya kazi ya kitaalam kama hivyo ya utanganzaji mpira au hata habari unapaswa uwe na uelewa wa namna ya kutamka majina.
Hivyohivyo kwa watu wa external affairs wao ndo kabisa inabidi watafute watu husika wa ubalozi na kijifunza.
Hata mimi nimegundua kuna tatizo kubwa sana la uvivu wa kujifunza na kutaka kuelewa na mtu kukataa kukubali kuwa unakosea mahala.
Ukishakubali unakosea basi unakuwa tayari kujifunza lakini utakuta mtangazaji kusika anajiunga na JF na anaanza kubisha mpaka kuchwee.
Mkuu nisaidie utamkaji wa jina la beki kisiki wa Bayern Munich Matts Hummels. Hilo jina la pili huku kwetu kila mtu anatamka kivyake
Hawajaenda shule siku hizi kama unakipaji unakuwa mtangazaji
Angalia tu tv ya mawingu
Hivi lafudhi ndio lahaja au ?
Maana hapa nataka niseme kitu.
Martin Tyler na Peter Drury katika kusuma kwangu padi naskiaga wanasema,Huyu sijui huwa wanatamkaje "Wijnaldum"
Upo sahihi kabisa na nina kuunga mkono kwa asilimia mia,ila hapa ulitakiwa uongezee tamko "lugha moja" ili kuleta maana ya wazi zaidi.Variant au lahaja ni aina mbalimbali ya matamshi ya neno lakini hayaharibu maana.
Martin Tyler na Peter Drury katika kusuma kwangu padi naskiaga wanasema,
"Wainaldam"
Upo sahihi kabisa na nina kuunga mkono kwa asilimia mia,ila hapa ulitakiwa uongezee tamko "lugha moja" ili kuleta maana ya wazi zaidi.
Mfano lafudhi huwa imejikita sana katika mtoko wa sauti,mathalani ukimsikiliza mpare akiongea Kiswahili au mchaga utajua kutokana na sauti invyosikika na hii huwa ina athiriwa sana na maeneo husika kama ulivyosema.
Na lahaja inaingia katika lugha moja lakini lugha hiyo inakuwa ina zungumzwa katika mtindo tofauti hasa wa kimsamiati ukiambatana na mtoko wa herufi. Mathalani kuna lahaja ya Kimvita,Kiamu,Kipete,Kipemba,Kiunguja hizi zote ni lahaja za Kiswahili yaani wote wanazungumza Kiswahili,ila tofauti yao unaikuta katika matamshi kadhaa,kama sijapoteza kumbukumbu,mfano "Macho" kwa Kiamu hutamkwa "Mato" na mfano wake.
Nukta yangu ya msingi ni kumwambia yule niliye mnukuu kule juu,na ndio nilichokuwa nataka nikiseme ni kuwa "Lafudhi sio sababu ya kumfanya mtu ashindwe kutamka jina la watu wa lugha kando kwa ufasaha"
Martin Tyler na Peter Drury katika kusuma kwangu padi naskiaga wanasema,
"Wainaldam"
Wapolish hutamka "W" kama "V".....huyo jamaa ni Mpolish Sawa na Lewandowski hutamkwa "Levandoski".
Yaah ni Mholanzi (Dutch) nimejichanganya tu. But Wadachi na Wapolish (Wapoland) Wana mfumo unaofanana wa utamkaji wa majina yao hasa yenye herufi "w" ndani yake.Huyo ni mholanzi. Au wapolish ndio waholand
haha.Jim beglin na peter dury.
haha.
nmemaanisha watangazaji wote kutoka kwenye hizo title mbili za FIFA na PES wote hutamka sawa, "JIOJINO WAINALDAM"