Majina mengine unajifunza kwa kusikiliza wenye majina yao. Mfano Hughes inatamkwa Hyuz sasa utasikia mtangazaji anatamka hugiz/hagiz/hagez
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
Hii kitu nimewahi kuiona zaidi ya Mara mbili, Mfano mtangazaji badala ya kutamka "soul" kwa maana Seoul (Mji mkuu wa Korea kusini) mtangazaji anasema "seuli"Majina mengine unajifunza kwa kusikiliza wenye majina yao. Mfano Hughes inatamkwa Hyuz sasa utasikia mtangazaji anatamka hugiz/hagiz/hagez