Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

Mkuu Tanzania tunamatatizo mengi sana hilo nalo ni tatizo pia..

Darasa la kwanza mpaka la saba kiswahili mwanzo mwisho, ghafla tu unaanza form one kiingereza mwanzo mwisho hapo ndio mpaka unakua Professa lazima ukariri tu mwisho wa siku ukajibu mtihani.
 
Wafundisheni na hao Wazungu kutamka vizuri majina yetu ya Kibantu..

Sisi ndio wenye shida na wao mara kutwa kucha tunazungumzia habari zao na kutaja majina yao.. Kuanzia Ligi ya UK mpaka ya Urusi... Wao hawana shida na sisi maana kama mpira hawaangalii wa kwetu na wala hawafuatilii habari zetu mbaya zaidi wakija kwetu kuchimba dhahabu mkataba unaandikwa tena kwa kiingereza chao....
 
Sasa kama iliishia form 4 ya div 4 unatagemea huyo ndugu yako atatamkaje hayo maneno na hata kujua vichache tu kuhusu hayo mambo anayoyatangaza??
Chuo chenyewe kasoma Ilala Bungoni au Eagle kwa miezi 6 sasa kuna kipya unakitarajia hapo??
Jana nimemsikia mmoja ktk kipind cha michezo akidai Tottenham wamekiwakisha katika jiji la Ajax walipocheza na Ajax, nikajiuliza anataka kusema walicheza kule Canada ambako katika jiji la Ontario kuna town inaitwa Ajax?
Unaweza kujifunza kwa kusikia wenye hayo majina wanatamkaje, mfano Thierry Henry hata pale England hawatamki Kiingereza kama King Henry bali wanatamka Kifaransa kwasababu mwenye jina ni Mfaransa kawaambia linatamkwa Honrii
 
Hayo maneno ya maeneo ya ulaya na ugaibuni sio issue sana kwana hata wazungu wenyewe wakija kwetu maeneo yetu yanawashinda kutamka kinachoniudhi ni wale wanaoshindwa kutofautisha kati ya herufi L na R kwenye magari mathalani atatamka magali
Wazungu wanajitahidi kujifunza, ingawa kuna maneno huwa yanawashisha mfano Mwamba utawasikia wanajikakamua Mawamba
 
RRONDO nina mwalimu mmoja wa kizungu eti alinifundisha kutamka. Lester.

Ana asili ya kimasai lakini mama mdiye mzungu.. ila nadhani anajua kizungu maana namwamini.
Haraka haraka inasikika lester.
 
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
Hunishindi mimi, nakwazika mno!
 
watangazaji wa tanzania sehemu R wanaweka L tena haoni aibu: mfano anaringa wao analinga, rudini redioni wao ludini ledioni
 
Usishangae mkuu hata hao wenye majina hayo walikuja kwetu enzi hizo walishindwa kutamka majina ya maeneo yetu wakaharibu mpaka leo tunataja majina ambayo siyo asili yetu.

Mfano, Tabora, Njombe, Iringa, kwenye mito wameharibu na milima pia.
Hata hapo Nairobi wamasai halisia walikuwa wanapaita Nairobai. Kwa mwingereza ai ndio anavyotamka i. Ikawa Nairobi. Kwa huko Scandinavia wanatamka London kama inavyoandikwa ila mwingereza yeye anatamka Landan, kwa mfano.
 
Polisi, manesi, waalimu, watangazaji, wahudumu wa hoteli the list goes one....

Kibongo bongo makundi hayo ya watu yana sifa moja kielimu...naomba nisiendelee zaidi
 
eti jamani Tumblr inatamkwaje? Tumblr ni mtandao wa huko marekani sasa nimepewa assignment hapa na maboss kuhusu huo mtandao nawaza sijui niwatamkie TUMBILI ?
 
..inakera sana hasa ukizingatia kuwa hawa watu wanapata nafasi ya kusikika na wengi...jana nimemsikia yule mtangazaji (mwandishi?) Baby Kabaya kwenye mazishi ya Mzee Mengi akisema...." ....Hizo ni makaburi za familia..." badala ya ..." hayo ni makaburi ya familia..". Wanaonikera zaidi ni wale waosema..Nyimbo hii..badala ya wimbo huu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom