Mmang'ati
Senior Member
- Jan 8, 2011
- 184
- 49
- Thread starter
- #21
Haya ni matatizo ya kiisimu kulingana na mazingira aliyokulia! Wasukuma hawana (r) mhaya hana n'go! Soma lugha usiwasumbue watangazaji wetu wako poa.
Mkuu kuwaacha ni kuwaharibu na kuwachanganya watoto wanaowasikiliza na kufanya kazi ya walimu wetu mashuleni iwe ngumu maradufu.Mwalimu anatumia nguvu na muda mwingi kumfundisha mwanafunzi kutamka neno dhuluma baadae mtoto anasikia mtangazaji anatamka zuluma huoni kuwa tunamchanganya mtoto? Sina tatizo na lafudhi anayoitumia mtangazaji iwe ya kikurya,ya pwani au ya kihehe lakini kwenye matamshi ya maneno haivumiliki.Maneno kama "SAMANI"yapasa litumike kumaanisha furniture na wala si value kama ambavyo watu hawa hupotosha hasa kwa kuzingatia kuwa ITV ni SUPER BRAND NO 1 TV STATION