Watangazaji/maripota hawa walipataje kazi?

Mmang'ati

Senior Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
184
Reaction score
49
Ni muda mrefu sasa kumekuwa na wimbi la watangazaji au maripota wa television na radio wasiomudu kutamka maneno ya kiswahili wanapokuwa wakiripoti/wakitangaza au wakisoma hasa taarifa ya habari.Hii imekuwa kero unapomsikia ripota anatamka maneno mfano bizaa(bidhaa),feza(fedha)samani(thamani)taalifa(taarifa)n.k.Kifupi matumizi ya r/l,th/s na dh/z ni kero iliyopitiliza kwa hawa watu kwani huondoa ladha ya matamshi ya kiswahili.Sasa swali ninalojiuliza ni vp watu hawa walifaulu usaili(interview)ktk vituo husika na zaidi wanaendelea kuharibu tu.Walifaulu vp mitihani yao tangu shule za msingi mpaka kupata kufikia elimu ya juu? Je maboss hawawasikizi wakawarekebisha? on job trainning hakuna?hata daily briefing pia hakuna?Enyi waandishi nguli mlioko humu jamvini tusaidieni kujadili.
 
Nakerwa na hao watu mkuu nafikiri ni utaahira fulani hivi. Mimi kwa ufahamu wangu nilidhani inalazimika ufaulu masomo ya lugha kuwa mtangazaji. Sasa mtangazaji anasema 'watoto wametekelezwa' na hata hashtuki kuona ameosea.

Mwingine yupo Radio One (Japo nahisi kama amejirekebisha manake kitambo kidogo sijasikia uharo wake), yeye huyu hajui anachoongea. 'Timu ya soka ya .....jana ilifanikiwa kufungwa mabao ma3 kwa bila ktk michuano.....'

Lakini ndio kichefuchefu cha nchi yetu. Nimetoka kuweka uzi mwingine kwa madudu niliyoyakuta kwenye website ya VETA. Pamoja na kwamba wanajinadi kuwa wanafundisha web designing na development, site yao ni kichefuchefu utafikiri daftari la mtoto anayejifunza course ya computer
 
Hili ni janga kwa taifa letu.hatuhitaji matokeo ya mitihani kujua ubora wa elimu yetu.hii ni dalili iliyo wazi kabisa kuwa shule na vyuo vyetu ni "vijiwe" vya kukuzia umri.nahofia sana mustakbali wa taifa langu!
 
Nakerwa na hao watu mkuu nafikiri ni utaahira fulani hivi. Mimi kwa ufahamu wangu nilidhani inalazimika ufaulu masomo ya lugha kuwa mtangazaji. Sasa mtangazaji anasema 'watoto wametekelezwa' na hata hashtuki kuona ameosea.

Mwingine yupo Radio One (Japo nahisi kama amejirekebisha manake kitambo kidogo sijasikia uharo wake), yeye huyu hajui anachoongea. 'Timu ya soka ya .....jana ilifanikiwa kufungwa mabao ma3 kwa bila ktk michuano.....'

Lakini ndio kichefuchefu cha nchi yetu. Nimetoka kuweka uzi mwingine kwa madudu niliyoyakuta kwenye website ya VETA. Pamoja na kwamba wanajinadi kuwa wanafundisha web designing na development, site yao ni kichefuchefu utafikiri daftari la mtoto anayejifunza course ya computer

Yaani yupo mmoja itv halafu kila taarifa ya habari lazma aripoti sijui ametumwa? Hebu mwambieni hakuna neno bizaa....aagh inaboa sana.Hivi nyie mlio mahiri ktk kutangaza akina Mwaipaya,double G,Deo,Maulid hamyaoni haya mapung
 
Walugaluga wengi mjini, ndo maendeleo hayo.
 
Niko serious ITV mkalisheni kitako huyu ripota wenu otherwise msiendelee kujiita super brand....mlimpaje kazi huyu jamaa halafu ana bonge la mwili matamshi ya kiswahili anavurunda.Mambo gani haya kuweni wastaarabu itv muwekeni back ofice mpaka aive ndo aweze kuripoti.
 
Lafudhi ya kiswahili inatofautiana baina ya mtu na mtu kutokana asili zetu, ningejali kama mwandishi anakosea kuandika kiswahili lakini kulaumu matamshi ya mtu hii ni dalili mpya ya mtindio wa ubongo.
Yule reporter wa aljazeera Kamal Hyder mbona hajafukuzwa kazi kutokana na lafudhi yake ya peshawar acheni ungese, serukamba you, leteni hoja ambazo ni logical.
 
Haya ni matatizo ya kiisimu kulingana na mazingira aliyokulia! Wasukuma hawana (r) mhaya hana n'go! Soma lugha usiwasumbue watangazaji wetu wako poa.
 
Lafudhi ya kiswahili inatofautiana baina ya mtu na mtu kutokana asili zetu, ningejali kama mwandishi anakosea kuandika kiswahili lakini kulaumu matamshi ya mtu hii ni dalili mpya ya mtindio wa ubongo.
Yule reporter wa aljazeera Kamal Hyder mbona hajafukuzwa kazi kutokana na lafudhi yake ya peshawar acheni ungese, serukamba you, leteni hoja ambazo ni logical.
Huaelewa mada, mtoa mada hamaanishi lafudhi, anamaanisha utamshi wa herufi hata siku moja "feza" yaweza kuwa kitamkwa kingine cha fedha! "samani" thamani ni vitu tofauti usitetee hata ujinga, hapa si mjadala wa lafudhi kama ilivyo kiingereza cha waganda, wanaigeria, wahindi au waghana! hiyo inafahamika duniani kote. Ipe haki yake thread ili wahusika wajirekebishe
 
Ni muda mrefu sasa kumekuwa na wimbi la watangazaji au maripota wa television na radio wasiomudu kutamka maneno ya kiswahili wanapokuwa wakiripoti/wakitangaza au wakisoma hasa taarifa ya habari.Hii imekuwa kero unapomsikia ripota anatamka maneno mfano bizaa(bidhaa),feza(fedha)samani(thamani)taalifa(taarifa)n.k.Kifupi matumizi ya r/l,th/s na dh/z ni kero iliyopitiliza kwa hawa watu kwani huondoa ladha ya matamshi ya kiswahili.Sasa swali ninalojiuliza ni vp watu hawa walifaulu usaili(interview)ktk vituo husika na zaidi wanaendelea kuharibu tu.Walifaulu vp mitihani yao tangu shule za msingi mpaka kupata kufikia elimu ya juu? Je maboss hawawasikizi wakawarekebisha? on job trainning hakuna?hata daily briefing pia hakuna?Enyi waandishi nguli mlioko humu jamvini tusaidieni kujadili.

mleta maada acha upuuzi,taja majina ya hao wana habari
 
Huaelewa mada, mtoa mada hamaanishi lafudhi, anamaanisha utamshi wa herufi hata siku moja "feza" yaweza kuwa kitamkwa kingine cha fedha! "samani" thamani ni vitu tofauti usitetee hata ujinga, hapa si mjadala wa lafudhi kama ilivyo kiingereza cha waganda, wanaigeria, wahindi au waghana! hiyo inafahamika duniani kote. Ipe haki yake thread ili wahusika wajirekebishe

utakuwa miongoni mwa wale wanafunzi wa kawambwa mliochora zombie kwenye mitihani halafu serikali ikawapa marks za bure.
 
Zao la maskan za ccm. Merit, merit we assassinated merit for nepotism all the way to upper echelon.
 
sasa msipowataja watajijuaje na kujirekebisha.........?
 
Lafudhi ya kiswahili inatofautiana baina ya mtu na mtu kutokana asili zetu, ningejali kama mwandishi anakosea kuandika kiswahili lakini kulaumu matamshi ya mtu hii ni dalili mpya ya mtindio wa ubongo.
Yule reporter wa aljazeera Kamal Hyder mbona hajafukuzwa kazi kutokana na lafudhi yake ya peshawar acheni ungese, serukamba you, leteni hoja ambazo ni logical.

No wonder unaitwa MBWA.Mada inazungungumzia matamshi ya maneno sijazungumzia lafudhi,ikiwa umeshindwa kutambua tofauti hiyo ambayo kimsingi ni elimu ya darasa la tatu instead unakuja jukwaani kuporomosha matusi ukijiona mjanja ilhali umejivua nguo hadharani.Kaa chini tafakari usije kuwa zombie zaidi ya watoto wa kawambwa mada ni juu ya namna ya kutamka maneno kiusahihi na wala si lafudhi ya kiswahili.Ni uchafu kwa ripota kutamka neno bizaa badala ya bidhaa la pengine ni wewe J. Chacha umeamua kujilinda.
 
Back
Top Bottom