Watanganyika Wanaridhika na Muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanganyika Wanaridhika na Muungano?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMBOTA, Mar 17, 2012.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kati ya maswala ambayo yamenichukua mda kuyatafiti pasipo majibu ni hili la watanganyika kutolalamikia muungano tofauti na wazanzibar ambao wako mstari wa mbele kuonyesha kosoro zake na kulilia maboresho, swali gumu zaidi ni ama la watanganyika wameridhika nao? au wanangoja muda mwafaka wa kutoa kero zao pia?
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Mar 17, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Muungano upi?
  Ninavyojua Nyerere aliondoka na Muungano wake
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Wanazo kero japo si nyingi kama za upande wa pili.

   
 4. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2012
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mtanganyika wa kawaida hana habari na muungano maana katika maisha yake ya kila siku hauhitaji na wala haumuongezei chochote. Wazanzibari wa kawaida na viongozi wao siwezi kuzungumza kwa niaba yao ninachojua wao ni kila siku kulalamika kuhusu muungano. Huenda kwao una manufaa fulani vinginevyo wasingekuwa wanalalamika.
   
 5. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Aisifuye mvua ujue imemnyea.
  Na siri ya kaburi aijuaye maiti.
  Na siri ya maiti aijuaye mwosha??
   
 6. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hakuna watu wanaouchukia huu muungano kama Watanganyika tukianza na mimi mwenyewe.
  Kinachofanya watanganyika wasiupigie kelele ni maneno ya Mwalimu Nyerere (laana) kwa atakayeuvunja. Tunasubiri wazenji wauvunje ili waondoke na laana zao. Kila siku naomba mungu yatimie ya kuvunjika kwa muungano.
   
 7. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mtanganyika. Sijaona umuhimu wa huu muungano. Ah mi nshachoka! Hata tukiachana. Kwanza haya maisha ya Tanganyika na Z'bar hayafanani.
   
 8. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Sisi tunauona na kama ni muungano wenye kasoro, wao wauona muunganao kama kisingizio cha kuendelea kuwatawala kisiasa,kiuchumi na kifikra. Jambo ambalo lina ukweli mwingi ndani yake, ukweli usio ruhusiwa kuongelewa hadharani.
   
 9. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Kambota na Wana JF,
  Nafikiri Wazanzibar na Wapemba wanalalamika kwa sababu wanaona wanaonewa,ndio maana hata Watanganyika muda hatuna na hatutaki kupata laana ya waasisi wa Muungano, dhambi ya sisi Watanganyika na wao Wazanzibari itawatafuna kwa walioanza kuuvunja Muungano. Tatizo lingine huo Muungano kufanywa siri
  Nawakilisha


   
 10. P

  Praff Senior Member

  #10
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  The muungano is there because it is there full stop.
   
 11. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mi naomba saana huu muungano usiwepo, kwa upande wangu siuhitaji kwa kuwa naona ni kitu cha kulazimishwa tuu, Hata hawa viongozi wetu sidhani kama wanaukubali huu muungano, ni wa kinafikinafiki. Naona tuachane kwa muda and then tukiona kuna manufaa tujadiliane kwa upya!!!
   
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  mie kama mtanganyika siridhiki kabisaaaaaa na huu muungano
   
 13. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,952
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  sitegemei muungano kuwepo hadi 2015. Ingawa kikwete kashaingia gharama ya vitambulisho. Wazenji hebu vunjeni mzaliane na kujaza ka-ardhi kenu kadogo. Jussa ana tools zote, ni kum-switch tu
   
Loading...