Watanganyika tukoje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanganyika tukoje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tutor B, Jul 7, 2012.

 1. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Jamani ndugu zangu tufike hatua tutambue madudu ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi na kuishinikiza iondoke madarakani pasipo kusubiri 2015. Madai ya madaktari si yao tu, yanahusu hata sisi raia, mazingira mazuri ya kazi ndo itakuwa ponapona yetu. Nakumbuka miaka ya 90 hospital za serikali zilikuwa hazipokei majibu ya vipimo toka maabala binafsi, lakini siku hizi unaambiwa kapime kwanza ulete majibu ndo uhudumiwe,
  Wajawazito wanaambiwa huduma kwao ni bure - madawa hakuna maospitalini. Hivi tunasubiri na wake zetu wagome kupewa mimba, tukose watoto tuzeeke tufe wabaki wale walobatika kuiba twiga, tembo na madini yetu ndo tujue kuwa Serikali haina uchungu na wananchi wake.
  Angalia hili la mgomo wa walimu, sisi walala hoi tunaangaika kupeleka watoto twition kwa kuwa kipato chetu ni kidogo, watoto wa wenye nacho wako kwenye shule za private ambazo nazo pia ni vituo vya kukusanyika tu watoto. Performance za huko ni maajabu tu. Walimu wanaofundisha ni product ya mgomo baridi, hawana maadili, ni mashalubalo, masister du, wale walimu wa miaka ya 90 wakiisha kwenye system hali ya elimu itakuwa mbaya kuliko.
  Mtoto anafika form four hajui hata kuandika jina lake kwa ufasaha!
  TAFAKARINI HAYA, JADILINI, UNGANENI NA CHADEMA, HATA KAMA NI KADA WA CCM KAMA SABODO, TUUTOKOMEZE UOZO HUU ULIOKO MBELE YETU. VINGINEVYO WATOTO TULIOWAZAA WATAKUJA KUTUPIGA MAKOFI KWA KUSHINDWA KUWAJIBU MASWALI WATAKAYOTUULIZA.
  Hivi mtoto wako akikuuliza kuwa wakati mafisadi wanaifilisi nchi na wewe ulikuwa mtu mzima ulichukua hatua gani? Utampa jibu lipi?

  Tumefikia hatua ya kuimbiwa nyimbo za mafumbo na makada wa CCM? Angalia kibwagizo hiki...
  "Tunachukua, tunaweka wah"
  Wanamaanisha kuwa wanachukua rasilimali za taifa wanaweka wanakokujua. Alafu maskini wanaoimba wao wanachukua khanga, t-shirt na kofia wanaweka majumbani kwao wakisubiria mikutano yao isiyokuwa na maana wavae tu ilimradi rangi ya kijani na njano ionekane wale wali na manyama basi!

  WATANGANYIKA JAMANI AMKENI.... INANIUMA SANA!
   
 2. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  ... Tatizo watanganyika hawana "ari" kama wapemba resilience kwao ndogo sana na hapa ndipo Nyerere alipofanikiwa sana kwa watanganyika mpaka leo mnasindindwa kujua asali na kuita asali mnadhani sukari guru ni asali, aamkeni kumekucha na hii ni gari ya mwisho (katiba mpya) msipoipata Tanganyika yenu basi mjue mpaka dunia itakwisha mtakuwa chini ya himaya ya Tanzania mtakuwa koloni letu Zanzibar. kama ilivyokuwa hapo kabla kwa Bwagamoyo, Bandari Salama, Mafia, na Pemba Msumbuiji na Mombasa
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
 4. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Nimekusoma kaka! Hivi matatizo tuliyonayo Tanganyika ni kweli yote yanasababishwa na katiba mbovu? Au ni watanganyika wenyewe kukosa uelewa wa haki zao Kama Mtumbatu alivyosema!

  Enzi niko shule tulikuwa na maadui wawili wa Tanzania, Ujinga, maradhi na Umaskini. Ujinga ndo hadui mkubwa zaidi kwa sababu amefanya yaibuke maadui mengine - Si ujinga kuuza mali za wenzako alafu pesa ukapekea nje ya nchi. Unaiba ukijua wazi kuwa hautaishi milele.
  Maisha aloishi Baba wa Taifa ni yakuigwa, lakini wajinga walimwondoa, na kesi hawana.
   
 5. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Ujinga na woga ndo tatizo, watu wanaogopa utafikiri wamezaliwa kuishi milele.
   
 6. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ukiwa pori ikinyanganya usafiri, inakuwaje. Katiba ndugu yangu ikichakachuliwa huweza hata kuleta machafuko makubwa sana. Sasa hii katiba tunayoirasimu ni ya nchi gani, Tanzania, Zanzibar au Tanganyika. Na ujue zote zina mahusiano. Ndio tumeanza tunataka tanganyika kwanza, muungano baadaye. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/282291-katiba-tanganyika-irudi-kwanza-ndipo-rasimu-ya-katiba-ifuate.html
   
Loading...