Watanganyika tuamkeni...

Mimi nipo Zenje na nimeangalia hizi harakati zao hapa kwakweli zinatisha huwezi kuamini na inasemekana kuna baadhi ya viongozi walio wengi wameitaka SMZ wawache kama walivo kwa7bu wanadai haki yao ya kuwa huru.

Na pia alikuja Mkapa wiki 2 hv na kumtaka Shein awasimamishe hawa jamaa lakini Mr Ben alijibiwa kuwa huu sio wakati wa kulazimishana, ikiwa na maana kama Wazenji hawataki muungano waachiwe na harakati zao.

Lakni pia wamekuwa wakikashifu Watanganyika hadharani na SMZ hawajahi kuwakemea, na ikitokea kiongozi yoyte kuwakemea basi anajibiwa hadharani kwa maneno makali na hakuna hatua inayochukuliwa.
Angalia picha hii ni moja kati ya mikutano mingi wanayoifanye hapa Zenji, na hapo wanaulizwa" MNAUTAKA MUUNGANO AU HAMUUTAKI NA WAZENJI WANAJIBU HATUUTAKI"
X9ZzMrKysrKyGYxKysr63v+A+rqzDh0zjuEAAAAAElFTkSuQmCC
Michenzani, Zanzibar.

Na wao wameazimia kuwalazimisha wawakilishi kuisindikiza SMZ waandae kura ya maoni ya kuukubali au kuukataa muungano, na trhe 26April watakuwa na maandamano makubwa ya kuukataa huo muungano.
Jee sisi Watanganyika tumejipanga vpi? Na kwanini tuko kimya namna hii wenzenu tunadhalilishwa na hawa jamaa!!!
Au tunaogopa ? Nawasilisha............................
 
Dalili za udhaifu wa muungano ilionekana tangu zamani mtindo wa funika bovu umetumika miaka mingi sana. Kama kweli tuna dhani tuko serious na mustakabali wetu basi tuamue leo kilicho bora kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae. Hiccups za muungano mimi nimeanza kuzifeel tangu nikiwa form two wakati wa mtitkisiko na mchafuko wa hali hewa siasa za zanzibar jumbe alipofurushwa kwenye madaraka na pengine hata kabla ya hapo watu walona ufa huu. Kumix zenji na bara imeshindikana. Ni vizuri tuamue moja liwalo na liwe muungano basi tena . Haiwezekani mtu anayeupinga muungano eti anapewa madarka halafu anatulia kama maji ya mtungi. Hebu tutumie peoooooooooples power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
Kama wanajadili sheria ya ubaguzi wa ajira basi vice president aondoke kwanza kabla sheria hiyo haijaanza kutumika.
Ugumu ninaouona mimi ni pale wazenji wanaposhiriki kikamilifu juu ya masuala ya muungano pamoja na mambo ya tanganyika hili jambo linaniumiza kweli. Tulipokuwa tunasoma vyuo enzi hizo za 1980s tulianza kuchangia huduma za elimu kwa kulipa ada lakini wenzetu wazenji walikuja kama scholarships free of charge na kichele kila mwezi. Sisi tutabeba dhamana ya wazanzibari hadi lini. Umeme hawalipi kama sisi. Limzigo la nini. Kikwete, mwinyi, mkapa tuambieni huu mzigo wabara tutaubeba kwa faida ipi hasa na wazenji wana hasara ipi inayowafanya walipwe fadhila za vyeo na nafuu ya huduma kama umeme??????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
ilianza na abdurahman babu, alipoonekana hataki muungano pamoja na mambo mengine, akapoozwa kwa kupewa uwaziri bara. Hata makamu wa kwanza wa mjomba hakuwa anapenda muungano, akapoozwa, sasa hivi swaaafi pamoja na wengine wengi mnao wajua! jusa siyo tu kama ni mbaguzi, lakini anajua wazi akisimamia kauli yake sio tu kama atopewa uwaziri bara, pengine kwenye serikali ya umoja huko zanzibar..(kama bado). Kwahiyo washajua dili, aliyepo kwenye kijinafasi japo tu cha uwakilishi, akisema na kukaza kuwa hataki muungano, fukuza hao wabara warudi kwako, basi tanzania bara watatetemeka na kutafuta jinsi ya kumpoza huyo mtu kwa cheo au fedha....!

Lazima tufahamu kuwa jusa pamoja na ubaguzi wake hayupo pekee, anao wananchi nyuma yake ambao wangependa wamsikie hivyo, kama anavyoonwa shujaa kwa kutamka wabara watoswe ajira visiwani hadharani, kama alivyompinga tibaijuka katika mipaka. Hata katika baraza la wawakilishi jusa aliposema wabara waniwe, nusu walimwunga mkono, na walio mpinga walieleza wasiwasi wao kuwa wazenji waliopo bara nao watatoswa, lakini siyo kwa ajili ya sababu kuwa wabara wasinyimwe fursa za ajira kwakuwa ni wenzetu.

Seriakali ya jamuhuri, upande wa bara, inatumia gharama kubwa kwa kile kinachoitwa kuudumisha muungano, ambao upande wa pili (zanzibar) hawautaki. Na kama wananchi wangekuwa wanautaka, hakika wangewakemea kina jusa. Wazenji wengi wapo peponi huku, wakituuzia vimeo vya electoniki, wana mashamba na majumba, maduka ya jumla na rejareja, vibanda vya urojo na maziwa, mawaziri, polisi n.k lakini hali ni tofauti kwa wabara walioko zenji.

hivi, nterest ya tanzania bara juu ya huu muungano ni nini? nini watanzania tunafaidika na huu muungano? Au pengine, faida yake ni vyeo vinavyozaliwa katika ishu ya kero na jinsi ya kuitatua? Hivi ni kweli kuwa wao wanalipa bei ya chini ya unit moja ya umeme na maji ukilinganisha na bara? Hivi ni kweli pass mark zao hupandiswa ili kupewa ufaulu katika usahihishaji wa mitihani ili amfikie mtanzania bara? Wapo kwenye bunge letu, lao wabunge wetu wapo? Jusa anataka rais ajaye wa tanzania (mwinyi aliwahi) atoke zanzibar (bado haina shida hata wakija mia), lakini hatujamsikia anataka lini rais wa zanzbar ajaye atokee bara? Hivi, walivyochoma vibanda vya biashara vya wa bara walioko zenji, hawajui kuwa ndugu zao wana vibanda vya kuchaji simu mitaani kwetu d'salaam? Tayari walishaunda katiba yao ambayo haiitambui katiba iliyopo, tena bila kuhusisha upande mwingine wa muungano, lakini hii ya huku inayofanyiwa marekebisho wao wametoa wajumbe 15, je marekebisho ya katiba hii itahusisha na marekebisho ya katiba mpya ya zanzibar? Kwasababu ili twende sawa lazima katiba zitambuane.

Kwa kifupi, kama kuna faida zozote kwa tanzania bara juu ya huu muungao, tuelimishwe ili tuupende na kuuenzi. Kamati ya jaji warioba watuelimishe katiba mpya ya zanzibar itaoana vipi na katiba hii mpya tunayoitegemea, hasa kama kuna haja ya kuwa na muungano. Tanzania tumejitolea sana kwa ukombozi na uhuru wa nchi nyingi za africa, ikiwapo zanzibar, matokeo yake raia wetu wananyanyaswa katika nchi hizo, sasa basi inatosha kufanywa mazuzu, ni wakati sasa wa kujijenga wenyewe na kuacha unafiki wa kuita hawa wenzetu, huku tukitambua fika kabisa wao hawatutambui sisi kama wenzao. Haya na kwa manufaa ya wajukuu wa wajukuu zetu tusio wafahamu.

Kibanga msese
 
poa waacheni wajitoe kwenye muungano maana faida ilikuwa kwao,sasa wanakubali hasara laiti wangejua umuhimu wasingesema hivyo.TANGANYIKA NI YE2,TANZANIA NI YE2 NA ZANZIBAR NI YAO.VIVA TG,TZ
 
Na ninawaambia mkiung'ang'ania huu muungano mtatukoma wazanzibar;
moja ya makubaliano tutakayoyaweka kwenye katiba
1) Usawa wa nafasi za kiserikali kama mawaziri makatibu wa kuu
2) usawa wa mapato yatokanayo na gesi,madini hata kama hatuna znz
3)Uraisi wa mpokezano tena kwenye katiba

NA MWAKA HUU MTAJUTA, SI KILA ALILOLOFANYA BABA YENU WA TANGANYIKA LILIKUWA SAHIHI.

KWANINI MNANG'ANG'ANIA MUUNGANO WAKATI HATUUTAKI? NI KWELI BEN KAJA KUOMBA VIONGOZO WA ZNZ WASIJITOE NA AKAAHIDI MATATIZO NA KERO ZOTE ZITASHUGHULIKIWA TENA ZITAWEKWA KWENYE KATIBA .
HUU NI UDHAIFU MKUBWA MLIONAO WADANGANYIKA!
 
Back
Top Bottom