Watanganyika tuamkeni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanganyika tuamkeni...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by K.Msese, Apr 11, 2012.

 1. K

  K.Msese JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,467
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Ilianza na Abdurahman Babu, alipoonekana hataki muungano pamoja na mambo mengine, akapoozwa kwa kupewa uwaziri Bara. Hata Makamu wa kwanza wa mjomba hakuwa anapenda muungano, akapoozwa, sasa hivi swaaafi pamoja na wengine wengi mnao wajua! Jusa siyo tu kama ni mbaguzi, lakini anajua wazi akisimamia kauli yake sio tu kama atopewa uwaziri bara, pengine kwenye serikali ya umoja huko Zanzibar..(kama bado). Kwahiyo washajua dili, aliyepo kwenye kijinafasi japo tu cha uwakilishi, akisema na kukaza kuwa hataki muungano, fukuza hao wabara warudi kwako, basi Tanzania bara watatetemeka na kutafuta jinsi ya kumpoza huyo mtu kwa cheo au fedha....!

  Lazima tufahamu kuwa Jusa pamoja na ubaguzi wake hayupo pekee, anao wananchi nyuma yake ambao wangependa wamsikie hivyo, kama anavyoonwa shujaa kwa kutamka wabara watoswe ajira visiwani HADHARANI, kama alivyompinga Tibaijuka katika mipaka. Hata katika baraza la wawakilishi Jusa aliposema wabara waniwe, nusu walimwunga mkono, na walio mpinga walieleza wasiwasi wao kuwa wazenji waliopo Bara nao watatoswa, lakini siyo kwa ajili ya sababu kuwa WABARA WASINYIMWE FURSA ZA AJIRA KWAKUWA Ni WENZETU.

  Seriakali ya Jamuhuri, upande wa Bara, inatumia gharama kubwa kwa kile kinachoitwa kuudumisha muungano, ambao upande wa pili (zanzibar) hawautaki. Na kama wananchi wangekuwa wanautaka, hakika wangewakemea kina JUSA. Wazenji wengi wapo peponi huku, wakituuzia vimeo vya electoniki, wana mashamba na majumba, maduka ya jumla na rejareja, vibanda vya urojo na maziwa, mawaziri, polisi n.k lakini hali ni tofauti kwa wabara walioko zenji.

  Hivi, nterest ya Tanzania Bara juu ya huu Muungano ni nini? Nini Watanzania tunafaidika na huu Muungano? Au pengine, faida yake ni vyeo vinavyozaliwa katika ishu ya kero na jinsi ya kuitatua? Hivi ni kweli kuwa wao wanalipa bei ya chini ya unit moja ya umeme na maji ukilinganisha na bara? Hivi ni kweli pass mark zao hupandiswa ili kupewa ufaulu katika usahihishaji wa mitihani ili amfikie mtanzania bara? Wapo kwenye bunge letu, lao wabunge wetu wapo? Jusa anataka rais ajaye wa Tanzania (Mwinyi aliwahi) atoke Zanzibar (bado haina shida hata wakija mia), lakini hatujamsikia anataka lini rais wa Zanzbar ajaye atokee Bara? Hivi, walivyochoma vibanda vya biashara vya wa bara walioko Zenji, hawajui kuwa ndugu zao wana vibanda vya kuchaji simu mitaani kwetu D'salaam? Tayari walishaunda katiba yao ambayo haiitambui katiba iliyopo, tena bila kuhusisha upande mwingine wa muungano, lakini hii ya huku inayofanyiwa marekebisho wao wametoa wajumbe 15, je marekebisho ya katiba hii itahusisha na marekebisho ya katiba mpya ya zanzibar? Kwasababu ili twende sawa lazima katiba zitambuane.

  KWA KIFUPI, KAMA KUNA FAIDA ZOZOTE KWA TANZANIA BARA JUU YA HUU MUUNGAO, TUELIMISHWE ILI TUUPENDE NA KUUENZI. KAMATI YA JAJI WARIOBA WATUELIMISHE KATIBA MPYA YA ZANZIBAR ITAOANA VIPI NA KATIBA HII MPYA TUNAYOITEGEMEA, HASA KAMA KUNA HAJA YA KUWA NA MUUNGANO. Tanzania tumejitolea sana kwa ukombozi na uhuru wa nchi nyingi za Africa, ikiwapo Zanzibar, matokeo yake raia wetu wananyanyaswa katika nchi hizo, sasa basi inatosha kufanywa MAZUZU, ni wakati sasa wa kujijenga wenyewe na kuacha unafiki wa kuita hawa wenzetu, huku tukitambua fika kabisa wao hawatutambui sisi kama wenzao. Haya na kwa manufaa ya wajukuu wa wajukuu zetu tusio wafahamu.

  Kibanga Msese
   
 2. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  mkuu eti sisi ni wa amani na utulivu
   
 3. T

  Topical JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Watanzania bara ndio mdudu gani?

  Umeshindwa kusema sisi wa Tanganyika; utaweza kudai haki wewe; maweeee
   
 4. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,057
  Likes Received: 1,091
  Trophy Points: 280
  Tunataka Tanganyika yetu Bwana
   
 5. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Katiba ya sasa hairekebishwi bali katiba mpya inaandikwa!!
   
 6. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  We want our own country TANGANYIKA, muungano wa serekali mbili, kisha serekali ya shirikisho kwisha!
   
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,318
  Likes Received: 2,604
  Trophy Points: 280
  kuna kitu wale binadamu wanaoishi Zanzibar wanaoojiita Wazanzibar wanatakiwa wajiulize, nalo si swali gumu sana bali ni hili, "Asili yao ni wapi?",laiti kila mmoja akipatia kujijibu then watatambua ya kwamba wote ni wahamiaji tu...
   
 8. dallazz

  dallazz Senior Member

  #8
  Apr 11, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  jusa hautaki muungano
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu umeeleza vizuri kuhusu viongozi wanaopiga mdomo kuhusu Muungano kuwa lengo lao ni madaraka, ila kidogo nitofautiane na wewe kuwa Muungano tuna faida nao si wabara tu bali hata Wazanzibari. Faida ya kwanza ni kuwa sote ni no muungano , no TANZANIA binafsi nalipenda sana jina TANZANIA kuliko jina lolote litakalo kuwa mbadala wa hilo, pili Amani mkuu, no MUUNGANO no amani kwani Maadui wanaweza kutumia ZANZIBAR kujificha ili kutushambulia au wakajificha Bara wakashambulia ZANZIBAR na mengine mengi , tunaweza kuendelea kuyaorodhesha. MUUNGANO UDUMU.
   
 10. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Jambo la msingi kabisa ni kwamba tuipiganie Tanganyika yetu irudi. Pili, Muungano huu uvunjwe and then tunaweza kushirikiana na Wazanzibar kama tunavyoshirikiana na Wakenya, waganda, etc. Only a fool can tolerate this union!
   
 11. J

  JAY2da4 JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Jusa ndo shetani gani?Anyway huu muungano ufe tu,tunakimbizana na EA ili hali muungano umetushinda,kuwaunganisha waafrika ni kazi kweli kweli.
   
 12. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kweli watanganyika ni watu wa ajabu sana. Tumekubali kuuza uhuru wetu kwa wazanzibar. Ni kweli kabisa wazanzibar wanatunyanyasa kwa mambo mengi sana kama ukiwa kwenye aridhi yao.
  Inakuwaje eti mtanganyika anashindwa kumiliki aridhi ya zanzibar lakini mzanzibar anamiliki aridhi ya tanganyika kiulaini? Ifike wakati watanganyika waache woga wao na waliseme hili tena kwa kupaza sauti ya juu kabisa.
  Kiujumla huu muungano hauna manufaa yeyote kwa sasa bali ni kivuli cha watawala wetu kujigawia madaraka serikalini. Hapa tukitaka muungano wa dhati na wenye tija basi hatuna budi kukaa meza moja na kukubaliana aina ya muungano tunaoutaka. Vinginevyo ni kuendelea kupoteza muda na kitu kisichokubalika na wengi na pia hakina tija kwa maendeleo ya tanganyika na zanzibar.
  Binafsi naona kama wazanzibar wanaendesha kampeni ya ubaguzi nje nje kwa kuwa wanajua watanganyika hawana sauti ya kupinga huo ubaguzi. Kibaya zaidi viongozi wengi wa tanganyika ni woga wa kuisema tanganyika. Wengi wa viongozi wa tanganyika tulionao ni watu wa kuburuzwa tu.
  Imefika wakati sasa na watanganyika wakaamka kwenye hili, hapa namaanisha waitetee na kupigania Tanganyika yao. Ni aibu sana kwa mtu kupoteza utaifa wako, eti leo hii kuna mzanzibar lakini hakuna mtanganyika. Eti mtanganyika ananyimwa haki yake ya kujiita mtanganyika bali analazimishwa ajiite mtanzania bara.
  Hivi huyu mtanzania bara ni mtu gani? Nijuavyo katika tanzania kuna mzanzibar na mtanganyika kwa kuwa nchi zao za zanzibar na tanganyika ziliungana. Kuungana kwa nchi haimaanishi kuwa watanganyika wanapoteza utanganyika wao na wazanzibar wanabaki na uzanzibar wao!
  Namaliza kwa kusema poleni sana watanganyika kwa manyanyaso mnayopata kutoka kwa hao mnaodhani kuwa umeungana nao kumbe si kweli. Ukweli ni kwamba mmetawaliwa na wazanzibar na kama hamtachukua hatua madhubuti mtatawaliwa na kubaguliwa milele yaani kizazi na kizazi chenu!
   
 13. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Mkuu Msese, kwa niaba ya Magamba nakuonya uache uchochezi mara moja Tz ni nchi ya AMANI. Hata hivyo naomba nikuulize ni muungano upi unaouelezea wewe? Ninachojua mimi baada ya uhuru wa Tanganyika, kwa ujinga wa mitanganyika kwa hiyari yetu tulikubali kuwa chini ya ukoloni mambole wa wazanzibari. Ndiyo maana wazanzibari wanaruhusiwa kuwa marais wa mitanganyika, lakini vitanganyika haviruhusiwi kugombea hata usheha kule. Mtanganyika ndivyo ilivyo inathamini sana amani kuliko haki yao!
   
 14. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Muungano huu uliundwa kwa sababu ya makubalino ya watu wa wawili! Hauna baraka ya umma.
   
 15. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hilo ni wazo zuri la kupenda nchi yenu tanganyika, kama sisi tunavyopenda zanzibar yetu.
  Wazanzibar wamechoshwa na muungano huu wa kikoloni, kwa hiyo kuendelea kuwazimisha munakaribisha kuongezeka kwa chuki dhidi ya watanganyika.

  Na kama kuwepo kwa wazanzibar huko tanganyika ndio kisingizio cha kuendelea kuidhalilisha zanzibar, basi subirini ije hiyo tume zanzibar tuukatae halafu na wao wataamua kama watakaa tanganyika au watarudi, hayo watasuka au kunyoa.

  Kama munataka muungano wa haki, basi tujue tunaungana na nani, sio kama sasa hivi hatujui tumeungana na nani, sasa tumechoka na hakuna wakutuzia.

  "muungano ni kama koti likikubana unalivua"
   
 16. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #16
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hilo la maadui kujificha, ni rahisi zaidi Kenya, Uganda, DRC, Zambia, Malawi, Rwanda na Burundi. Hii hua naaita sababu ya kitoto, au changa la macho. Tufate sababu za kiutu uzima kidogo.
   
 17. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Ukiwa na familia kubwa 'extended family' hutaki atoke hata mchun gaji wa ng'ombe, Zanzibar ndiyo sifa ya Kaya yetu kubwa hatutaki watoke japo hawana faida saaana!!!
   
 18. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tanganyika tuliikomboa wenyewe kwa mkoloni. Nani kasema tumelala!!!!!!!!
   
 19. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #19
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mimi nadhani muungano una faida kubwa sana kwa wapemba kuliko sisi, huoni walivyojaa hapa dar? wanafaidi, bora waondoke warudi kwao pemba
   
 20. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #20
  Apr 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  nadhani tumesahau kwamba siku hizi vita hawajifichi vinatumwa vifaa..
   
Loading...